Al-Muminoon
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
قُلْ مَنۢ بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ 88 سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ 89
{88-89} Kisha akaendelea na kukiri kwao kile kilicho cha jumla zaidi kuliko yote hayo, na akasema: "Sema: ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu?" Yaani, Ufalme wa kila kitu kutoka ulimwengu wa juu na ulimwengu wa chini, kile tunachokiona na kile tusichokiona, na ufalme ni hali iliyozidishwa kwa maana ya mfalme. "Naye ndiye anayewalinda" waja wake kutokana na shari na huwaondolea yanayowaudhi, na anawahifadhi kutokamana na yanayowadhuru, "wala hakilindwi asichotaka." Yaani, hawezi mtu yeyote kulinda juu ya Mwenyezi Mungu na wala hazui shari ambayo amekadiria Mola, bali pia haponyi yeyote mbele yake ila kwa idhini yake. "Watasema (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu." Yaani, watakiri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mmiliki wa kila kitu,anayelinda ambaye hakilindwi asichotaka." "Sema" kwao wanapokiri kwa jambo hilo la lazima kwao, "Basi vipi mnadanganyika;" yaani, basi akili zenu zinakwenda wapi mlipowaabudu wale mliowajua kuwa hawana ufalme wala sehemu ya utawala, na kwamba hawakuwa na uwezo kwa kila jambo, na mkaacha uaminifu kwa Mmiliki Mkuu na Mwenye Nguvu anayesimamia kila kitu? Basi akili zilizowaongaza kwenye haya si chochote ila ni kurogwa, na bila ya shaka, Shetani aliziroga kwa yale aliyowapambia, akawarembeshea na akapotosha ukweli kwao, na akaziroga akili zao, kama wachawi walivyoroga macho ya watu.