Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ لَكُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ ٱسْتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَسَوَّىٰهُنَّ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ 29
(29) Yani amekuumbieni katika hali ya kuwafanyia wema na rehema vyote vilivyomo katika ardhi kwa manufaa yenu, na starehe na mazingatio. Na katika aya hii tukufu kuna dalili kwamba hali ya asili (kanuni ya msingi) katika vitu ni kwamba vinaruhusiwa na ni safi. Kwa sababu (aya hii) ilisimuliwa katika muktadha wa kuonyesha neema; hivyo machafu yanatoka kwa hili. Kwa sababu uharamu wake unachukuliwa kutokana na maana ya aya hii, na kujua makusudio yake, na kwamba aliviumba kwa manufaa yetu; hivyo lenye madhara lipo nje ya hilo. Na katika ukamilifu wa neema yake ni kwamba alitukataza machafu ili kutusafisha. Na kauli yake: (29) Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. (Neno) “Istawa” linatokea katika Qur-ani kwa maana tatu: Mara huivuki kwa msaada wa herufi (harf); hivyo linamaanisha “ukamilifu na utimilifu”, kama katika kauli yake kuhusu Musa: “Na Musa alipofika utu-uzima baraabara” Na mara nyingine linakuwa na maana ya “kuwa juu” na “kuinuka” na hilo ni ikiwa litavukishwa na “alaa (juu)” kama katika kauli Yake Mtukufu “Ar-Rahman (Mwingi wa Rehema) aliyetawala juu ya Kiti cha Enzi” “Ili make vizuri juu ya migongo yao”. Na wakati mwingine linakuwa na maana ya “kukusudia” kama vile linapovukishwa na “ilaa (kuelekea)” kama ilivyo katika aya hii. Yani yeye Mtukufu alipoumba ardhi, akaelekea kuziumba mbingu “na akazifanya mbingu saba.” Basi akaziumba na akaziimarisha na akazifanya vilivyo Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. Kwa hivyo, anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Na anajua mnayoyaficha na mnayoyatangaza. Anajua siri na kilichofichika zaidi (kuliko siri). Na mara nyingi anaunganisha baina ya uumbaji wake na kuthibitisha elimu yake, kama ilivyo katika aya hii, na kama katika kauli yake: “Asijue aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?” Kwa kuwa, uumbaji wake wa viumbe ni dalili ya kutosha juu ya elimu yake, hekima yake, na uwezo wake.