Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sourate 2

Al-Baqara

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Verset 210

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأْتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِى ظُلَلٍ مِّنَ ٱلْغَمَامِ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَقُضِىَ ٱلْأَمْرُ ۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ 210

Na haya, ndani yake yamo onyo kali na tishio ambayo nyoyo hutetemeka kwa sababu yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Je, wanangoja hao wanaozunguka katika ardhi wakifanya ufisadi, wanaofuata nyayo za Shetani, wanaoitupilia mbali amri ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa Siku ya Malipo kwa matendo. Ambayo imejazwa mahangaiko, dhiki na mambo ya kutisha yenye kutia wasiwasi katika nyoyo za madhalimu ambayo kwayo yatawafika malipo mabaya wafanyao ufisadi? Na hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atazikunja mbingu na ardhi, na sayari zitatawanywa, jua na mwezi vitakunjwa, na malaika watukufu watateremka na wawazunguke viumbe. Na Al-Bari (Muumba mwanzilishi), [Mwenye baraka], Mtukufu atateremka “katika vivuli vya mawingu” ili apambanue kati ya waja wake kwa hukumu ya uadilifu. Kwa hivyo mizani itawekwa, na vitabu vitaenezwa. Na nyuso za watu wa furaha (waliofaulu) zikakuwa nyeupe, nazo nyuso za watu wa taabuni zitakuwa nyeusi. Na watu wa heri watatenganishwa na watu wa shari (uovu), na kila mmoja atalipwa kwa matendo yake. Basi hapo, dhalimu atajiuma mikono yake atakapojua uhakika wa hali yake. Na Aya hii na mfano wake ni dalili ya dhehebu la Ahlul-Sunnah wal-Jama`ah, ambao huthibitisha sifa za hiari (za Mwenyezi Mungu). Kama vile istiwaa (kuinuka juu), kushuka, kuja na mfano wa hizo miongoni mwa sifa ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kuhusu nafsi yake. Au Mtume wake rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ndiye aliyetoa habari juu yake. Wao huthibitisha kwa namna ambayo inalingana na utukufu wake na ukuu wake, bila ya kufananisha, wala kupotosha. Kinyume na Al-Mu’atila na mfano wao miongoni mwa wale wanaozipinga sifa hizi. Na wanazifasiri aya kwa sababu ya hilo tafsiri ambazo Mwenyezi Mungu hakuziteremshia hoja yoyote. Bali uhakika wake ni kukashifu katika ubainisho wa Mwenyezi Mungu, na ubainisho wa Mtume wake na kudai kuwa maneno yao ndiyo yanayotokana nayo uongofu katika mlango huu. Na hawa hawana daili yoyote ya kimaandiko bali hata hawana dalili ya kiakili. Ama dalili ya kimaandiko, wao kwa hakika walikiri kwamba maandiko yaliyokuja ndani ya Kitabu na Sunna, maana yake ya dhahiri bali ya moja kwa moja inaashiria kwenye dhehebu la Ahlul-Sunnah wal Jama`ah. Na kwamba inahitaji ili ziashirie kwenye dhehebu lao batili zinapaswa kuondolewa katika maana zake za dhahiri na ziongezewe ndani yake na zinapunguzwe. Na hili, kama unavyoona, haliridhii yule ambaye ndani ya moyo wake kuna uzito wa chembe moja ya imani. Ama dalili ya kiakili, basi hakuna kitu katika akili kinachoashiria kukanusha sifa hizi. Bali akili inaashiria kuwa mtendaji ni mkamilifu zaidi kuliko asiyeweza kutenda. Na kwamba kitendo chake Mtukufu kinachohusiana na nafsi yake na kuhusiana na viumbe wake ndiyo ukamilifu. Wakidai kuwa kuzithibitisha kunaashiria kufanana na viumbe wake, basi wataambiwa: Kuongea juu ya sifa zake kunafuata kuongea juu ya dhati yake. Kwa hivyo, kama vile Mwenyezi Mungu ana dhati ambayo dhati nyinginezo hazifanani nayo, basi Mwenyezi Mungu ana sifa ambazo sifa nyinginezo hazifanani nazo. Sifa zake zinafuata dhati yake, na sifa za viumbe wake zinafuata dhati zao. Kwa hivyo, hakuna chochote katika kuzithibitisha ambacho kinalazimu mfanano kwa namna yoyote. Na vile vile inasemwa kwa mwenye kuthibitisha baadhi ya sifa na kukanusha baadhi, au alithibitisha majina na sio sifa: Ima uvithibitishe vyote kama Mwenyezi Mungu alivyovithibitisha, na Mtume wake alivyovithibitisha, au uvikanushe vyote. Hivyo, utakuwa unamkanusha Mola Mlezi wa walimwengu. Ama kuthibitisha kwako baadhi ya hayo na kukanusha kwako baadhi yake, huko ni kujipinga mwenye, na hutapata njia ya kutofautisha. Ukisema: Alichokithibitisha hakilazimu mfanano, basi Ahlul-Sunnah watakwambia: Na kuthibitisha mnayoyakataa hakulazimu mfanano. Ukisema: Mimi sielewi katika yale niliyoyakanusha isipokuwa mfanano, basi wanaokanusha watakuambia: Na sisi hatuelewi katika yale uliyothibitisha isipokuwa mfanano. Basi uliyowajibu kwayo wakanushaji, Ahlul-Sunnah watakujibu kwa hayo hayo kwa yale uliyoyakanusha. Jambo la msingi ni kwamba mwenye kukanusha kitu na akathibitisha kitu katika yale ambayo Kitabu na Sunnah viliashiria kuthibitishwa kwake. Basi huyo anajipinga mwenyewe, na wala hana dalili yoyote imara ya kisheria wala ya kiakili bali amehalifu yale ya kiakili na yale ya kimaandiko.