Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ فِىٓ أَيَّامٍ مَّعْدُودَٰتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِى يَوْمَيْنِ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ ٱتَّقَىٰ ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ 203
Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kumtaja Yeye katika siku zinazohesabiwa, ambazo ni zile siku tatu za Tashriiq baada ya Idi. Kwa sababu ya umaalumu wake na utukufu wake, na kwa kuwa matendo yaliyobaki ya Hijja hufanyika ndani yake na kuwa watu ni wageni wa Mwenyezi Mungu ndani yake. Na kwa sababu hii, imeharamishwa kufunga Saumu ndani yake. Kwa hivyo kumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake kuna umaalumu ambao hauko katika siku zinginezo. Na ndiyo maana Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema. “Siku za tashriiq ni siku za kula, kunywa, na kumtaja Mwenyezi Mungu”. Na inaingia katika hilo kumtaja Mwenyezi Mungu katika hizo siku, kumtaja wakati wa kutupa vijiwe kwenye Jamaraat, na wakati wa kuchinja, na utajo unaofanya baada ya swala za faradhi tu. Bali baadhi ya wanachuoni walisema: “Inapendekezwa mtu kufanya takbira isiyo na mipaka, kama inavyokuwa katika zile siku kumi za kwanza za Dhul-Hijja”. Na hili haliko mbali (na usawa). “Lakini mwenye kufanya haraka (akarejea) katika siku mbili.” Yani alitoka Mina kabla ya kuzama kwa jua katika siku ya pili (baada ya siku ya Idi), “basi hakuna dhambi juu yake. Na mwenye kukawia” kwa kulala huko (Mina) usiku wa kuamkia siku ya tatu (baada ya Idi) na kesho yake akatupa vijiwe kwenye Jamaraat, “pia hakuna dhambi juu yake”. Na huku ni kupunguziwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu [Mtukufu] kwa waja wake katika kuruhusu mambo hayo mawili. Lakini inajulikana kwamba ikiwa mambo mawili yanaruhusiwa, basi (jambo) la nyuma ndilo bora zaidi, kwa sababu lina ibada nyingi zaidi. Na kwa kuwa huenda ikafahamika kutokana na kukanusha dhambi kuwa ni kukanusha dhambi katika hilo lililotajwa na mengineyo. Na ukweli ni kwamba dhambi imekanushwa kwa aliyetanguliza na aliyechelewesha peke yao. Akazuia hilo (la kukanusha dhambi) kwa kauli yake, “kwa mwenye kumcha Mungu”. Yani alimcha Mwenyezi Mungu katika mambo yake yote na hali za Hijja. Kwa hivyo, mwenye kumcha Mwenyezi Mungu katika kila kitu, basi akapata kukanushiwa dhambi katika kila kitu. Na mwenye kumcha katika kitu na siyo katika kitu kingine, malipo yake yanakuwa ya aina sawa na matendo yake. “Na mcheni Mwenyezi Mungu” kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na maasia yake. “Na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake,” na awalipe kwa matendo yenu. Kwa hivyo, mwenye kumcha, atapata malipo ya uchamungu kwake. Na yule asiyemcha, atamuadhibu adhabu kali kabisa. Hivyo basi, kujua malipo, ni miongoni mwa sababu kubwa zaidi zenye kusababisha kumcha Mwenyezi Mungu. Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akahimiza kwamba hilo lijulikane.