Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَلَا تَقُولُوا۟ لِمَن يُقْتَلُ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمْوَٰتٌۢ ۚ بَلْ أَحْيَآءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ 154
(154) Alipotaja Mwingi wa baraka, Mtukufu amri ya kutafuta msaada kwa subira katika hali zote, akataja mfano wa yale ambayo msaada wa subira unatumika ndani yake. Ambayo ni jihadi katika njia yake. Nayo ndiyo matendo ya utiifu ya kimwili bora zaidi, na lililo gumu zaidi kwa nafsi kwa sababu ya ugumu wake yenyewe. Na kwa sababu inapelekea kuua na kukosa uhai ambao wale wanaoitaka hii dunia wanautaka ili kupata maisha na mahitaji yake. Hivyo basi, chochote wanachokitenda ni kukifanyia juhudi na kukizuilia yenye kuipinga. Na inajulikana kuwa kipenzi hakiachiwi na wenye akili timamu isipokuwa kwa ajili ya kipenzi kilicho juu na kikubwa kukiliko. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuuawa katika njia yake, kwamba alipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi. Na dini yake iliyo dhahiri, na si kwa lisilokuwa hayo miongoni mwa malengo. Basi yeye kwa hakika hajakosa uhai mpendwa, lakini alipata uhai mkubwa na kamili zaidi kuliko mnavyofikiria na kuchukulia. Basi Mashahidi, “169. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. 170. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. 171. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini”. Basi je, kuna kubwa zaidi kuliko huu uhai ambao unajumuisha ukaribu na Mwenyezi Mungu Mtukufu? Na kufurahia kwao riziki yake ya kimwili katika vyakula na vinywaji vyenye ladha nzuri? Na riziki ya kiroho, ambayo ni furaha, ambayo ni bishara njema na kuondolewa kwa kila hofu na huzuni? Na huu uhai wa Barzakh (kaburini) ni makamilifu zaidi kuliko uhai wa duniani. Bali Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alijulisha kuwa roho za mashahidi ziko ndani ya ndege wa kijani kibichi, wanaokwenda kunywa kwenye mito ya Peponi. Na wanakula katika matunda yake, na wanarudi kukaa kwenye taa zinazoning'inia kwenye Kiti cha Enzi. Na katika Aya hii kuna himizo kubwa zaidi juu ya kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kushikamana na subira juu yake. Na lau kuwa waja wangehisi malipo ya waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakuna ambaye angebaki nyuma katika hilo. Lakini ukosefu elimu ya yakini kamili ndiyo iliyotuliza hima, na ikamzidishia usingizi mwenye kulala; na ikapoteza malipo makubwa na ngawira. Kwa nini isiwe hivyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “hakika Mwenyezi Mungu amenunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa.” Wallahi (Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu,) lau kuwa mtu angekuwa na nafsi elfu moja zikawa zinakwenda nafsi baada ya nafsi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, halingekuwa kubwa zaidi kuliko haya malipo makubwa. Ndio maana mashahidi, baada ya kushuhudia katika thawabu za Mwenyezi Mungu na malipo yake mazuri, hawatamani isipokuwa kurejeshwa hapa duniani ili wauawe katika njia yake mara baada ya mara. Na katika Aya hii, kuna dalili ya furaha ya Barzakh na adhabu yake, kama maandiko mengi yalivyosimulia hilo.