Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Sourate 16

An-Nahl

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Versets 45–47

أَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخْسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ ٱلْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ 45 أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِى تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ 46 أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ 47

{45 - 47} Huku ni kuhofisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wenye kukufuru na kukadhibisha na aina mbalimbali za maasia kwamba, anaweza kuwachukua kwa adhabu katika hali ya kughafilika kwao hali ya kuwa hawahisi. Ima awachukue kwa adhabu ya kutokea juu yao, au kutokea chini yao kwa kuwadidimiza au mfano wake. Na ima iwajie huku wako katika harakati zao na shughuli zao hali ya kuwa hawafikirii adhabu kabisa. Na ima huku wana hofu juu ya adhabu. Basi hawawezi kumshinda Mwenyezi Mungu katika hali miongoni mwa hali hizi zote. Lakini wao wako chini ya mshiko wake, nywele za mbele ya vichwa vyao ziko mkononi mwake. Lakini hawaadhibu kwa sababu yeye ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu. Hawaharakishii adhabu waasi, bali huwapa muhula, na salama, na kuwaruzuku, ilhali wao wanamuudhi yeye na wanawaudhi marafiki wake. Lakini pamoja na hayo, Yeye hufungulia milango ya toba, na anawaita waachane na mambo mabaya ambayo yanawadhuru, na anawaahidi kwa hilo heshima kubwa sana, na msamaha kwa dhambi walizofanya. Basi na astahi muhalifu Mola wake Mlezi kwamba awe anateremkiwa na neema zake kila wakati ilhali maasi yake nayo yanapanda kwa Mola wake Mlezi kila wakati. Na ajue kwamba Mwenyezi Mungu hupeana muhula na wala hapuuzi. Na kwamba anapomchukua, anamshika mshiko wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo. Basi na atubie kwake, na arejee kwake katika mambo yote. Kwa maana Yeye ni Mwenye huruma kubwa, Mwenye kurehemu. Basi na mtu aharakishe, tena aharakishe kuziendea rehema zake pana, na wema wake wa jumla, na kushika njia zifikishazo katika fadhila za Mola wake Mlezi, Mwingi wa kurehemu. Tazama! Nazo ni kumcha Yeye, na kutenda yale anayoyapenda na kuyaridhia.