At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ جَـٰهِدِ ٱلْكُفَّارَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ ۷۳
{73} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake -rehema na amani zimshukie -: "Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki." Yaani, tia juhudi kubwa katika kufanya jihadi dhidi yao, kuwawia mgumu ikiwa hali itahitaji ugumu juu yao. Na kufanya jihadi huku kunaingia ndani yake kufanya jihadi kwa mkono na kwa kufanya jihadi kwa hoja na ulimi. Kwa hivyo, mwenye kujitokeza miongoni mwao kupigana vita, yeye atapigwa vita kwa mkono, na ulimi, upanga na mkuki. Na yule atakayekuwa chini ya Uislamu kwa ahadi ya ulinzi au agano,basi yeye atafanyiwa jihadi kwa hoja na ushahidi, na atabainishiwa mazuri ya Uislamu na maovu ya ushirikina na ukafiri. Basi haya ndiyo waliyo nayo katika dunia hii, "na" ama katika Akhera, basi makazi yao ni "Jahannamu." Yaani, makazi yao ambayo hawatatoka humo, "na hapo ndipo pabaya zaidi pa kuishia."