At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ٱئْذَن لِّى وَلَا تَفْتِنِّىٓ ۚ أَلَا فِى ٱلْفِتْنَةِ سَقَطُوا۟ ۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌۢ بِٱلْكَـٰفِرِينَ ۴۹
{49} Yaani, miongoni mwa wanafiki hao yuko anayeomba ruhusa ya kubaki nyuma na akatoa udhuru mwingine wa ajabu. Akasema, "Niruhusu" katika kubaki nyuma, "wala usinifitini" katika kutoka. Kwani ikiwa nitatoka, na nikawaona wanawake wa Banu Al-Asfar, sitawezi kuwavumilia mbele yao. Kama alivyosema hivyo Aljaddu bin Qais. Na makusudio yake - Mwenyezi Mungu amweke mbali na heri - ni kujionyesha na unafiki. Kwamba nia yangu ni njema; kwa maana katika kutoka kwangu kuna majaribu, na kujiweka mbele ya uovu, na katika kutotoka kwangu kuna salama na kujiepusha na uovu. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akibainisha uongo wa kauli hii "kwa yakini wao hivyo wamekwisha tumbukia katika fitina," kwani ikiwa itachukuliwa kwamba msemaji huyu ni anasema ukweli katika makusudio yake, basi katika kusalia kwake nyuma kuna uovu mkubwa zaidi na majaribu makubwa zaidi ya uhakika. Nao ni kumuasi Mwenyezi Mungu na kumuasi Mtume wake na kufanya dhambi kubwa kwa ujasiri, na uwongo mkubwa. Na ama kutoka kwenda, basi ni madhara madogo kwa kulinganisha na kusalia nyuma. Kwani, hayo ni ya kudhaniwa tu pamoja na kwamba msemaji huyu makusudio yake ni kusalia nyuma, si lingine. Basi ndiyo maana akawaahidi adhabu kwa kauli yake, "Na hakika Jahannam imewazunguka makafiri" hawana pa kutokea humo, wala kimbilio, wala ukombozi, wala wokovu.