At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَأَذَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوْمَ ٱلْحَجِّ ٱلْأَكْبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِىٓءٌ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُۥ ۚ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِى ٱللَّهِ ۗ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ۳
{3} Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliwaahidi Waumini ya kuinusuru dini yake, na kuliinua neno lake, na kuwaangusha maadui zao miongoni mwa washirikina ambao walimtoa Mtume na wale waliokuwa pamoja naye kutoka Makka kutoka katika Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu na wakawahamisha kutoka kwenye yale waliyokuwa wakiyadhibiti katika ardhi ya Hijaz. Mwenyezi Mungu akamnusuru Mtume Wake na waumini mpaka alipoifungua Makka na akawadhalilisha washirikina, na Waumini wakawa ndio watawala na wenye ushinda juu ya makazi hayo. Kwa hivyo Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie akamuamrisha mtangazaji wake kwamba atangaze siku ya Hija Kubwa, nayo ni siku ya An-Nahr wakati watu wamekusanyika, muislamu wao na kafiri wao kutoka katika bara Arabia lote kuwa atangaze kwamba Mwenyezi Mungu yuko mbali na washirikina, yeye na Mtume wake. Kwa hivyo, hawana kwake ahadi na agano lolote. Kwa hivyo popote watakapopatikana, watauawa. Na waliambiwa: Msiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wenu huu! Na huo ulikuwa mwaka wa tisa wa Hijra, na Abu Bakr as-Siddiq Mwenyezi Mungu amridhie alikuwa ndiye aliyewaongoza watu katika Hijja. Na binamu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi mungu ziwe juu yake ndiye aliyetangaza umbali huo Siku ya Nahr, yani Ali bin Abi Talib Mwenyezi Mungu amridhie. Kisha Yeye Mtukufu akawatia moyo washirikina kutubia na akawahofisha dhidi ya kuendelea na ushirikina. Kwa hivyo akasema, "Kwa hivyo, mkitubu, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkigeuka, basi jueni kuwa nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu." Yaani, hamtampotea, bali mko katika mshiko wake, na anaweza kuwapa waja wake Waumini mamlaka juu yenu. "Na wabashirie wale waliokufuru adhabu chungu." Yaani, chungu, ya kutisha katika dunia hii kwa kuuawa, na kutekwa mateka, na kufukuziliwa mbali, na Akhera kwa Moto, na hapo ndipo pahali pabaya zaidi pa kutulia.