At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَقَدْ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ فِى مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْـًٔا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ ٱلْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ ۲۵
Yeye Mtukufu anawakumbusha waja wake Waumini juu ya nusura yake kwao katika maeneo mengi katika maeneo ya kukutana na maeneo ya vita, na mapambano, hata katika siku ya Hunain ambayo shida iliwawia kubwa mno, na wakaona kutosaidiana, na kukimbia jambo lililofanya ardhi kuwa finyu kwao pamoja na ukunjufu wake na upana wake. Na hilo ni kwamba Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie alipoiteka Makka, akasikia kwamba Hawazin wamekusanyika ili kupigana naye vita, kwa hivyo akawaendea yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika masahaba zake ambao waliiteka Makka na wale waliosilimu miongoni mwa wale walioachiliwa huru katika watu wa Makka. Na walikuwa elfu kumi na mbili, nao washirikina walikuwa elfu nne. Kwa hivyo, baadhi ya Waislamu wakajivuna kwa sababu ya wingi wao, na baadhi yao wakasema: Hatutashindwa leo kwa sababu ya uchache. Kwa hivyo walipokutana wao na Hawazin, wakawashambulia Waislamu mshambulio mmoja, basi wakashindwa, hakuna yeyote aliyekuwa anageuka kumtazama mwenzake, na hakubaki pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - isipokuwa karibia wanaume mia moja ndio waliobaki imara pamoja naye. Na wakawa wanapigana na washirikina, naye Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akawa anamkimbiza nyumbu wake kuelekea upande wa washirikina huku akisema: "Mimi ndiye Nabii, si uongo. Mimi ndiye mwana wa Abdul-Muttalib." Na alipoona kutoka kwa Waislamu kile alichokiona, akamwamuru Al-Abbas bin Abdul-Muttalib kwamba aite katika Ansari na Waislamu wengineo, naye alikuwa wa sauti kubwa sana, kwa hivyo akawaita, "Enyi wenza wa Samura! Enyi watu wa Surat Al-Baqarah!" Kwa hivyo, walipoisikia sauti yake, wakajumuika kujumuika kwa mwanamume mmoja, kisha wakapigana na washirikina, na Mwenyezi Mungu akawashinda washirikina ushindi mbaya sana, na wakaiteka kambi yao, na wanawake wao, na mali zao.
{25} Na hiyo ndiyo kauli yake Yeye Mtukufu, "Hakika Mwenyezi Mungu aliwanusuru katika maeneo mengi, na siku ya Hunayni." Nalo ni jina la mahali ambapo palikuwapo vita, kati ya Makka na Taif, "wakati wingi wenu uliwapa majivuno, lakini haukuwafaa kitu" kushindwa. Yaani, haukuwafaidi kitu kichache wala kingi, "na ardhi ikawa finyu kwenu" kwa sababu ya kile kilichowapata cha wasiwasi kubwa na huzuni mliposhindwa "pamoja na upana wake." Yaani, upana wake na ukunjufu wake "kisha mkageuka mkapeana migongo;" yaani, huku mmeshindwa.