At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
مَا كَانَ لِأَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا۟ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرْغَبُوا۟ بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِۦ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ ٱلْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٌ صَـٰلِحٌ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ ۱۲۰
{120} Yeye Mtukufu Anasema akiwahimiza watu wa Madina miongoni mwa Wahajiri, Ansari, na wale walio pembezoni mwake miongoni mwa Mabedui waliosilimu na wakawa Waislamu wazuri: “Haiwafailii watu wa Madina na Mabedui walio kando kando yao kusalia nyuma wasitoke na Mtume.” Yaani, haliwafailii hilo wala haliendani na hali zao. "Wala kujipendelea nafsi zao” katika kubakia kwake na kustarehesha kwake, na kutulia kwake “kuliko nafsi yake” tukufu na iliyo safi. Bali Nabii anastahili zaidi Waumini kuliko wao wenyewe. Basi ni juu ya Kila Muislamu ajitoe mhanga kwa ajili ya Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na amtangulize yeye mbele yake. Kwa hivyo, alama ya kumfanyia Mtume taadhima, na kumpenda, na kumuani kikamilifu ni kwamba wasisalie nyuma yake. Kisha akataja malipo yenye kumfanya mtu kutoka, akasema: "Hayo ni kwa sababu wao;" yaani, wale wanaofanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, "hakiwapati kiu, wala machovu, wala njaa, katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapowaghadhibisha makafiri,” kwa sababu ya kuingia katika makazi yao na kuziteka nchi zao. "Wala hakiwapati chochote kutokana na maadui” kama vile kushinda jeshi au kikosi cha kijeshi au kuchukua mali kama ngawira, “isipokuwa huandikiwa kuwa ni kitendo chema.” Kwa sababu, hizi ni athari zinazotokana na vitendo vyao. "Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya uzuri” ambao walifanya uzuri kwa kuharakisha kwao kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kutekeleza kwao yanayowapasa katika haki yake na haki ya viumbe wake. Basi matendo haya ni athari miongoni mwa athari za matendo yao.