پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Naba
سورهٔ ۷۸

An-Naba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۲۶–۳۰

جَزَآءً وِفَاقًا ۲۶ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ۲۷ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا كِذَّابًا ۲۸ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ كِتَـٰبًا ۲۹ فَذُوقُوا۟ فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ۳۰

{26 - 30} Na hakika walistahiki adhabu hizi mbaya ziwe ndiyo malipo yao mwafaka kwa mujibu wa matendo waliyoyafanya yaliyowapelekea huko. Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walijidhulumu nafsi zao wenyewe, na ndiyo maana akataja matendo yao yaliyowafanya kustahiki malipo haya, akasema: "Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hesabu (juu ya matendo yao)." Yaani, hawakuwa wakiamini kufufuliwa, wala kwamba Mwenyezi Mungu atawalipa viumbe kwa wema na uovu. Basi wakapuuza kuifanyia Akhera matendo, "Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu" wazi wazi, na zikawajia hoja zilizo wazi, lakini wakazipinga. "Na kila kitu" kichache, kingi, chema na kibaya "Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika" katika Ubao uliohifadhiwa. Kwa hivyo, wasidhanie wahalifu kuwa tumewaadhibu kwa madhambi ambayo hawakuyafanya, wala wasidhanie kuwa chochote katika vitendo vyao kitapotea au kusahauliwa uzito wa chembe. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyoogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote." Kisha akasema "Basi onjeni" enyi mnaokadhibisha adhabu hii chungu na hizaya ya daima. "Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!" Kwani adhabu yao hii itazidishwa kila wakati. Aya hii ndiyo aya kali zaidi miongoni mwa Aya zinazohusu ukali wa adhabu ya wakazi wa Motoni.