Al-Mursalaat
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
كُلُوا۟ وَتَمَتَّعُوا۟ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ ۴۶ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ۴۷ وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرْكَعُوا۟ لَا يَرْكَعُونَ ۴۸ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ۴۹ فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَهُۥ يُؤْمِنُونَ ۵۰
{46 - 50} Hili ni tishio na ni onyo kwa wale wanaokadhibisha kwamba hata wakila na kunywa katika dunia na wakastarehe na wakapuuza kufanya ibada za kuwaweka karibu na Mwenyezi Mungu, hao hakika ni wahalifu wanaostahiki kile wanachostahiki wahalifu, kwa njia ya kwamba starehe hizo zitawaisha na watabaki wakilaumiwa. Na miongoni mwa uhalifu wao ni kwamba wanapoamrishwa kuswali swala ambayo ni ibada ya heshima kabisa, na "wakiambiwa: Inameni! Hawainami" wanakataa kufanya hivyo. Basi ni uhalifu gani unaweza kuwa juu zaidi ya hili? Na ni ni kukadhibisha gani ambako ni zaidi ya huku? "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!" Na katika adhabu yao ni kuwa watafungiwa milango ya kuwezeshwa na watanyimwa kila la heri. Kwani wakiikadhibisha Qur-ani hii, ambayo ni kiwango cha juu kabisa cha kusadiki na yakini, "Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?" Je, wataamini batili ambao ni kama jina lake ambalo hauwezi kuleta shaka potofu yoyote, achilia mbali kuleta ushahidi? Au kuamini maneno ya mshirikina, mwongo kabisa wa dhaahiri? Kwa hivyo, hakuna kitu baada ya nuru iliyo wazi isipokuwa viza totoro, wala baada ya ukweli ambao ushahidi na uthibitisho wa uhakika umeuthibitisha ila uzushi mkubwa wa moja kwa moja na uwongo wa wazi - ambao haumfailii isipokuwa ile anayeufailia. Mwenyezi Mungu awaangamize, ni vipofu namna gani! Na ole wao, ni hasara gani yao kubwa hii na upotofu mkubwa ulioje! Tunamwomba Mwenyezi Mungu msamaha na salama. Hakika Yeye ni Mpaji mno, Mkarimu zaidi.
Imekamilika tafsiri.