پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Muzzammil
سورهٔ ۷۳

Al-Muzzammil

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۱–۵

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمُزَّمِّلُ ۱ قُمِ ٱلَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا ۲ نِّصْفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا ۳ أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلًا ۴ إِنَّا سَنُلْقِى عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا ۵

{1 - 5} Al-Muzzammil ni mtu aliyejivika nguo yake akajigubika kwayo. Na maelezo haya yalimtokea Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - Mwenyezi Mungu alipomtukuza kwa kumtuma kama mtume, na akaanza kwa kumteremshea ufunuo wake kwa kumpelekea Jibril, na akaona kitu ambacho hakuwahi kukiona mfano wake, na hakuna anayeweza kusimama imara mbele yake isipokuwa Mitume tu. Basi akapatwa na mfadhaiko alipomuona Jibril, amani imshukie, kwa hivyo akaja kwa ahali zake, akasema: 'Nifunikeni. Nifunikeni' huku akitetemeka viungo vyake. Kisha Jibril akamjia na kusema: 'Soma.' Akasema: 'Mimi siwezi kusoma.' Kwa hivyo akamfinya mpaka akamchosha mno, huku akimtaka kusoma. Basi yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akasoma. Kisha Mwenyezi Mungu akampa uthabiti na akaendelea kumteremshia ufunuo, mpaka akafikia kiwango ambacho hakuna hata mmoja katika Mitume aliyewahi kufika. Utakatifu ni wa Mwenyezi Mungu, ni jinsi gani hii ilivyo kubwa tofauti kati ya mwanzo wa unabii wake na mwisho wake! Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwongelesha kwa maelezo haya yaliyopatikana kutoka kwake mwanzoni mwa jambo lake. Basi akamuamuru hapa kufanya ibada zinazohusiana naye, kisha akamuamuru kuwa na subira katika kukabiliana na madhara kutoka kwa watu wake. Kisha akamuamuru kutangaza jambo hili na kulifanya hadharani katika kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu. Basi akamuamrisha hapa ibada yenye heshima kubwa zaidi, ambayo ni swala, na wakati wa uhakika na bora zaidi, ambao ni swala ya usiku. Na kutokana na rehema yake [Mwenyezi Mungu] ni kwamba hakumuamrisha kuswali usiku mzima, bali alisema: "Kesha usiku kucha, ila kidogo tu." Kisha akalikadiria hilo akasema: “Nusu yake, au ipunguze kidogo" ili iwe theluthi au mfano wake. "Au izidishe " hiyo nusu, ili karibia thuluthi mbili. "Na soma Qur-ani kwa utaratibu na utungo." Kwani kwa kusoma Qur-ani, yanapatikana mazingatio na tafakuri, na nyoyo husukumwa nayo, kufanya ibada kwa aya zake, na kujiandaa kikamilifu na kuwa tayari kwa ajili yake. Kwani alisema: "Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito." Yaani, tutakuteremshia Qur-ani hii nzito. Yaani, yenye maana kubwa, maelezo matukufu. Na kile chenye maelezo haya kinastahiki zaidi mtu kujitayarisha kwa ajili yake, kusomwa sawasawa na kutafakariwa yale yaliyomo.