Al-Haaqqa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ۳۰ ثُمَّ ٱلْجَحِيمَ صَلُّوهُ ۳۱ ثُمَّ فِى سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَٱسْلُكُوهُ ۳۲ إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ ٱلْعَظِيمِ ۳۳ وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ ۳۴ فَلَيْسَ لَهُ ٱلْيَوْمَ هَـٰهُنَا حَمِيمٌ ۳۵ وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ ۳۶ لَّا يَأْكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلْخَـٰطِـُٔونَ ۳۷
{30 - 37} Basi hapo itaamrishwa aadhibiwe, na wataambiwa Zabaniya wagumu na wakali mno: “Mshikeni! Mtieni pingu! Kisha mtupeni Motoni!" Yaani, mgeuzeni juu ya makaa yake na miale ya moto wake. "Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini" katika minyororo ya ya Motoni ambayo itakuwa moto sana kisha "mtatizeni." Yaani, iingizieni kwenye njia ya haja kubwa na itokee mdomoni mwake, na aning'inizwe humo asalie akiadhibiwa kwa adhabu hii mbaya zaidi. Basi hii ndiyo adhabu na mateso mabaya zaidi, na ni majuto makubwa magani haya, makemeo na lawama! Kwani sababu iliyomfikisha mahali hapa "ni kuwa hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu" kwa maana alikuwa ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi na kuwapinga Mitume wake, akiikataa haki waliyoileta, "wala hahimizi kulisha masikini." Yaani, hakuwa na rehema ndani ya moyo wake ya kuwaonea huruma maskini na wahitaji. Kwa hivyo, hakuwa akiwalisha katika mali zake mwenyewe, wala hakuwa akiwahimiza wengine kuwalisha. Kwa kuwa hakuwa na cha msukumo wa kufanya hivyo moyoni mwake. Haya ni kwa sababu chanzo cha furaha ni vitu viwili: kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, jambo ambalo msingi wake ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuwafanyia wema viumbe wa aina zote za wema, ambao mkubwa wake zaidi ni kuzuia mahitaji ya masikini kwa kuwalisha vile wanavyoweza kupata nguvu. Nao watu hawa hawamkusudii Mwenyezi Mungu peke yake wala hawafanyi wema, ndiyo maana wakastahili kile walichostahili. "Basi leo" siku ya Kiyama, "hana jamaa wa kumwonea uchungu" na kumfanyia uombezi ili aepuke adhabu ya Mwenyezi Mungu au apate malipo yake mazuri. "Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini" na akasema "Madhalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa." Na wala hatakuwa "na chakula ila usaha wa watu wa Motoni." Nao utakuwa moto sana, mchungu, wenye harufu mbaya, na wenye ladha mbaya, na hatakila chakula hicho cha kuchukiza mno "ila wakosefu" walioikosa njia iliyonyooka, na wakashika kila njia inayowafikisha kwenye Jahannamu; basi ndiyo wakastahiki adhabu iumizayo.