Al-Haaqqa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى لَمْ أُوتَ كِتَـٰبِيَهْ ۲۵ وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ ۲۶ يَـٰلَيْتَهَا كَانَتِ ٱلْقَاضِيَةَ ۲۷ مَآ أَغْنَىٰ عَنِّى مَالِيَهْ ۜ ۲۸ هَلَكَ عَنِّى سُلْطَـٰنِيَهْ ۲۹
{25-29} Hawa ndio watu wa mashakani. Watapewa vitabu vyao vyenye matendo yao maovu kwa mkono wao wa kushoto, ili kuwapambanua, kufedheha, na mmoja wao atasema kwa sababu ya wasiwasi yake kubwa na huzuni, "Laiti nisingeli pewa kitabu changu!" Kwa sababu kinanibashiria kuingia Motoni, na kwamba nitapata hasara ya milele. Natamani "nisingelijua nini hisabu yangu" nikawa nilisahaulika kabisa, na wala hata nisingefufuliwa ndiyo nikaulizwa hivi juu ya matendo yangu. "Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa." Yaani, laiti kifo changu kingekuwa ndicho kifo ambacho hakuna kufufuliwa baada yake. Kisha akageukia mali yake na mamlaka aliyokuwa nayo. Tazama, vyote hivyo vikawa ni msiba juu yake hakujitangulizia katika hivyo kwa ajili ya akhera yake, na wala havitomfaa chochote ikiwa atavitoa kwa ajili ya kukomboa kwavyo kutokana na adhabu. Hapo atasema: "Mali yangu hayakunifaa kitu" si katika dunia - kwa sababu sikujitangulizia ndani yake kitu - wala katika Akhera, na tayari wakati wa manufaa yake umeshapita. "Madaraka yangu yamenipotea." Yaani, yameondoka na kutoweka, na wala hawakuninufaisha kitu askari wala wingi (wa mali au wasaidizi) wala maandalizi ya hali ya juu wala heshima kubwa. Bali, yote hayo yalitoweka pamoja na upepo bure kabisa, biashara za faida zikatoweka kwa sababu yake, na badala yake zikaja wasiwasi kubwa, machungu na huzuni.