پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qalam
سورهٔ ۶۸

Al-Qalam

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۴۲–۴۳

يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ ۴۲ خَـٰشِعَةً أَبْصَـٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا۟ يُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمْ سَـٰلِمُونَ ۴۳

{42 - 43} Yaani, itakapofika Siku ya Kiyama, na zikatokea humo wasiwasi, mitetemeko na mahangaiko makubwa yasivyoweza kufikiriwa kwamba si kweli, na akaja Muumba kuhukumu baina ya waja wake na kuwalipa, kisha akaufunua muundi wake mtukufu ambao hakuna kinachofanana nao, na viumbe vikaona katika utukufu na ukuu wa Mwenyezi Mungu usioweza kuelezeka, hapo "na wataitwa kusujudu" kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Waumini waliokuwa wakimsujudia Mwenyezi Mungu kwa hiari yao watasujudu, nao waovu wanafiki watakwenda kusujudu, lakini hawataweza kusujudu. Migongo yao itakuwa kama nundu ya ng'ombe. Hawataweza kuinama, na malipo haya ni ya aina sawa na matendo yao (ya hapo awali). Kwani walikuwa katika dunia wakiitwa kumsujudia Mwenyezi Mungu, kumpwekesha na kumwabudu, hali wakiwa salama, bila ya kuwa na dosari yoyote, lakini wanalifanyia hilo kiburi na wanakataa. Basi usiulize kuhusu hali yao au hatima mbaya siku hiyo. Kwani Mwenyezi Mungu aliwakasirikia, na neno la adhabu likatimia juu yao, na mahusiano yao yakakatika kabisa, na majuto na kuomba udhuru havitawafaa Siku ya Kiyama. Basi haya ndiyo yanafaa kuisumbua mioyo kujitenga mbali na kutenda maasi na kuitia kufanya mema mapema katika muda wa uwezekano wa kufanya hayo.