پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Mumtahana
سورهٔ ۶۰

Al-Mumtahana

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذْ قَالُوا۟ لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُا۟ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ٱلْعَدَٰوَةُ وَٱلْبَغْضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَحْدَهُۥٓ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمْلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ ٱلْمَصِيرُ ۴

{4} “Hakika” enyi kundi la waumini, “mna mfano mzuri“ na kigezo chema na kufuata kutakaokufaeni “katika Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye” miongoni mwa Waumini; kwa sababu mliamrishwa kufuata mila ya Ibrahim mwongofu, “walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu.” Yaani, Ibrahim amani iwe juu yake na Waumini waliokuwa pamoja naye walipojitenga mbali watu wao washirikina na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi wakauweka wazi uadui wao, na wakasema: “umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi” na Hakuna wakati maalumu wala kikomo kwa uadui huo na chuki hii, lakini hilo ni “abadani” maadamu mnaendelea na ukafiri wenu, “mpaka mtakapomuamini Mwenyezi Mungu peke yake” Yaani: mkimwamini Mwenyezi Mungu peke yake, uadui na chuki vitatoweka na vitageuka kuwa mapenzi na kusaidiana. Basi nyinyi enyi Waumini mnao mfano mzuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye katika kusimamisha Imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu na mambo yanayofungamana na hayo, na matakwa yake, na katika kila jambo walilomuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwalo, “isipokuwa” jambo moja, nalo ni: “kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake” Azar, mshirikina, kafiri, mkaidi alipomwita kwenye imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu lakini akakataa. Ibrahim akamwambia: “Hakika nitakuombea msamaha” lakini mimi “similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu” lakini mimi namuomba Mola wangu Mlezi, labda nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi. Kwa hivyo, nyinyi msimfuate Ibrahim katika hali hii aliyomlingania mshirikina, kwani hamfai kuwaombea washirikina mkisema kwamba: ‘Hakika sisi ni wafuasi wa mila ya Ibrahim katika hilo.’ Kwa maana, Mwenyezi Mungu alitaja udhuru wa Ibrahim katika hilo katika kauli yake: “Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu wa ahadi aliyofanya naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye...” hadi mwisho wa Aya hii. Basi nyinyi mnao mfano mzuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye walipomuomba Mwenyezi Mungu na wakamtegemea na wakarejea kwake na wakakiri kutoweza kwao na kutofanya kwao ibada zingine vyema, waliposema: “Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea” katika kutuletea yale yenye manufaa kwetu na kutuepushe kutokana na yale yanayotudhuru, na tuna imani nawe katika hilo, ewe Mola wetu Mlezi, “na kwako tumeelekea” kwa kutubu, na kurudi katika utii na yote yenye kukuridhisha na yote yenye kutuweka karibu nawe. Sisi utafanya bidii katika hayo, na pia tunajitahidi kufanya mema, na tunajua kwamba tutarudi kwako, kwa hivyo tunajitayarisha kuja kwako, na kufanya yenye kutuweka karibu mno nawe.