Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذَا رَأَيْتَ ٱلَّذِينَ يَخُوضُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا۟ فِى حَدِيثٍ غَيْرِهِۦ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ ٱلشَّيْطَـٰنُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ ٱلذِّكْرَىٰ مَعَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ ۶۸
{68} Kinachomaanishwa na kuingilia Aya za Mwenyezi Mungu ni kusema yale yanayopingana na haki, kama vile kuboresha maneno batili, na kuyalingania, na kuwasifu watu wake, na kuipa mgongo haki, na kuikashifu na watu wake. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kwanza, na umma wake kwa kumfuata, wanapomwona mwenye kuziingilia Aya za Mwenyezi Mungu kwa kitu miongini mwa yale yaliyotajwa. Kwamba wajitenge nao, na wala wasihudhurie mikusanyiko ya hao wanaoziingia kwa batili, na wakaendelee katika hayo, mpaka watafute na kuingia katika maneno yasiyokuwa hayo. Na ikiwa ni katika maneno yasiyokuwa hayo, basi Katazo lililotajwa hapo juu linaondoka. Na ikiwa ni masilahi, basi hilo limeamrishwa. Na kama ni kisichokuwa hilo, basi halitakuwa na manufaa na wala halikuamrishwa. Na katika kushutumu kujiingiza kwa batili katika Aya za Mwenyezi Mungu kuna himizo la kutafiti, na kuzingatia, na kujadiliana kwa haki. Kisha akasema, “Na kama Shetani atakusahaulisha.” Yaani ikiwa utakaa pamoja nao kwa kusahau na kughafilika, "basi baada ya kutanabahi, usikae pamoja na kaumu madhalimu."Hili linajumuisha wale wanaojiingiza humo kwa batili, na kila mwenye kuzungumza jambo lililoharamishwa au mwenye kufanya kitendo kilichoharamishwa. Basi ni haramu kukaa na kuhudhuria wakati wa kuwepo kwa maovu ambayo mtu hawezi kuyaondoa. Katazo hili na kuharamisha ni kwa mwenye kukaa pamoja nao na hatumii kumcha Mwenyezi Mungu kwa namna kwamba, anashiriki nao katika kuzungumza maneno na vitendo vilivyoharamishwa au kuwanyamazia, na akaacha kuwakataza. Na akitumia kumcha Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kuwaamrisha kutenda mema na kuwakataza maovu na maneno ambayo yanatoka kwao, kwa hivyo hili linasababisha kuondoka kwa uovu huu au kuupunguza, basi huyu hapana ubaya juu yake wala dhambi, na ndiyo maana akasema: