Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قُلْ إِنِّى عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَكَذَّبْتُم بِهِۦ ۚ مَا عِندِى مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِۦٓ ۚ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۖ يَقُصُّ ٱلْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْفَـٰصِلِينَ ۵۷
{57} Na ama yale niliyo juu yake ya kumpwekesha mwenyezi Mungu na kumfanyia yeye tu matendo, basi hiyo hakika ndio haki ambayo ina ushahidi na hoja za mkato juu yake. Na "mimi nipo kwenye ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi; yaani, niko katika yakini iliyo wazi juu ya uhalali wake na ubatili wa kitu kingine chochote. Na huu ni ushahidi madhubuti kutoka kwa Mtume usiokubali kusitasita, naye ndiye shahidi mwadilifu zaidi kuliko [viumbe] wote. Basi Waumini wakauamini, na ikawabainikia katika usahihi wake na ukweli wake kulingana na yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu. Lakini nyinyi, enyi washirikina, “mnamkanusha,” na yeye hastahiki haya kutoka kwenu, wala haifailii ila kumsadiki. Na mkiendelea kukadhibisha kwenu huku, basi jueni ya kwamba adhabu itawafikia, hakuna kizuizi, nayo iko kwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye atakayeiteremsha juu yenu akitaka na apendavyo. Na mkiiharakisha, basi sina kitu mkononi mwangu katika jambo hili. "Hukumu si isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu." Basi Kama vile Yeye ndiye aliyehukumu kwa hukumu ya kisheria, akaamrisha na akakataza, basi Yeye hakika Atahukumu kwa hukumu ya malipo; basi atalipa mazuri na aadhibu kulingana na kile hekima yake inavyotaka. Kwa hivyo kuipinga hukumu yake kwa ujumla kunatupiliwa mbali. Kwa kuwa alikwisha iweka wazi njia na akawaambia waja wake haki ya kuwaambia ambako alimaliza kwa huko udhuru zao, na zikakatika hoja zao kwa hilo. Ili mwenye kuangamia na aangamie kwa hoja iliyo wazi, na anayeishi na aishi kwa hoja iliyo wazi. "Naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote," baina ya waja wake katika dunia na Akhera. Basi Atahukumu kati yao kwa hukumu ambayo hata yule aliyehukumiwa dhidi yake atamhimidi kwayo, na haki ikaelekezwa kwake.