Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوٓا۟ أَهَـٰٓؤُلَآءِ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنۢ بَيْنِنَآ ۗ أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَعْلَمَ بِٱلشَّـٰكِرِينَ ۵۳
{53} "Na hivi ndivyo tunavyowajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu?" Yaani, haya ni majaribio ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, alivyowafanya baadhi yao kuwa matajiri, na wengine wao kuwa maskini, na wengine wao kuwa waheshimiwa, na wengine wao kuwa wanyonge. Basi Mwenyezi Mungu akimpa imani masikini au mnyonge, hilo linakuwa jambo la majaribio kwa tajiri na mheshimiwa. Basi ikiwa makusudio yake ni haki na kuifuata, ataamini na kusilimu, na haitamzuia na hilo kushiriki pamoja na yule anayemuona kuwa chini yake kwa mali au heshima.Na ikiwa yeye si mkweli katika kutafuta haki, basi hili linakuwa ni kizuizi kinachomzuia kufuata haki, na wakasema wakiwadharau wale wanaowaona kuwa ni duni kuwaliko wao: "Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu?" Kwa hivyo, hili likawazuia kufuata haki kwa sababu ya kukosa kwao kuwa safi. Mwenyezi Mungu akasema katika kujibu maneno yao ambayo yanajumuisha kumpinga Mwenyezi Mungu kuhusiana na kuwaongoa watu hawa na kutowaongoa wao wenyewe: "Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanaoshukuru?" Ambao wanaijua neema na kuikiri na wanatekeleza yale inayoyataka miongoni mwa matendo mema. Basi Yeye Anawapa fadhila zake na neema zake juu yao kando na yule ambaye siyo mwenye kushukuru. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye hekima, na haweki fadhila zake kwa yule ambaye hazistahili, na hawa wanaopinga wana sifa hii. kinyume na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwa imani miongoni mwa masikini na wengineo. Wao kwa hakika ndio wenye kushukuru.