Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَمَا مِن دَآبَّةٍ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا طَـٰٓئِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِى ٱلْكِتَـٰبِ مِن شَىْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ۳۸
{38} Yaani, Wanyama wote wa ardhini na wa angani, miongoni mwa wanyama wa mifugo, na wanyama mwitu, na ndege, wote ni umma mfano wenu. Tuliwaumba kama tulivyowaumba nyinyi, na tukawaruzuku kama tulivyowaruzuku nyinyi, na mapenzi yetu na uwezo wetu yanatekelezeka kwao kama vile yanavyotekelezeka kwenu. "Hatukupuuza chochote katika Kitabu." Yaani, hatukupuuza wala kughafilika tukaacha kitu katika Ubao uliohofadhiwa. Bali vitu vyote - vidogo vyake na vikubwa vyake - vimenakiliwa katika Ubao Uliohifadhiwa jinsi vilivyo. Basi matukio yote yanatokea kama yalivyoandikwa na Kalamu. Na katika Aya hii kuna ushahidi kwamba lile andiko la kwanza lilijumuisha viumbe vyote. Na hili ni moja ya daraja za hukumu na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kwani ni daraja nne: Elimu ya Mwenyezi Mungu inayojumuisha kila kitu, na kuandika kwake kunakojumuisha vitu vyote vilivyopo, na mapenzi Yake na uwezo wake unaotekelezeka kiujumla juu ya kila kitu, na kuumba Kwake viumbe vyote, hata vitendo vya waja Wake. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa na Kitabu ni Qur’ani hii, na kwamba maana yake ni kama maana ya kauli yake Mola Mtukufu; "Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu." Na kauli yake, "Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa;" yaani, umma zote watakusanywa na kujumuishwa kwa Mwenyezi Mungu katika mahali pa Qiyama. Na katika mahali hapo pakubwa na pazito, atawalipa kwa uadilifu wake na ihsani yake, na atawapitishia hukumu yake ambayo kwayo atahimidiwa na wa mwanzo na wa mwisho. Wakazi wa mbinguni na wakazi wa duniani.