Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قُلْ تَعَالَوْا۟ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا۟ بِهِۦ شَيْـًٔا ۖ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَـٰنًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوٓا۟ أَوْلَـٰدَكُم مِّنْ إِمْلَـٰقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا۟ ٱلْفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا۟ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ۱۵۱
{151} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake-rehema na amani zimshukie-: "Sema" uwaambie hawa walioharamisha yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu: "Njooni niwasomee yale aliyowaharamishia Mola wenu Mlezi," kuharamisha kwa jumla kwenye kumuingiza ndani yake kila mmoja, kwenye kujumuisha maharamisho yote miongoni mwa vyakula, na vinywaji, na maneno, na vitendo. "Kwamba msimshirikishe Yeye na chochote;" yaani, si kidogo wala si kingi. Na uhakika wa kumshirikisha Mwenyezi Mungu ni kwamba kiumbe aabudiwe kama Mwenyezi Mungu anavyoabudiwa, au kutukuzwa kama anavyotukuzwa Mwenyezi Mungu, au kufanyiwa jambo ambalo ni katika mambo maalumu ya Umola na Uungu. Na ikiwa mja ataiacha shirki yote, anakuwa mpwekeshaji, mwenye kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika hali zake zote. Na kwa sababu ya hili ikawa haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwamba wamuabudu wala wasimshirikishe na chochote. Kisha akaanza na haki kubwa zaidi baada ya haki, akasema: "Na wazazi wawili wafanyieni uzuri," miongoni mwa maneno mema, mazuri, na matendo mazuri yapendezayo. Kwa hivyo kila neno na tendo lenye kuleta manufaa kwa wazazi wawili au furaha kwao, basi hilo ni katika uzuri. Na ikiwa uzuri utapatikana, basi uasi kwao unakosa kuwepo. "Wala msiwauwe watoto wenu" wa kiume na wa kike; "kwa sababbu ya umasikini." Yaani, kwa sababu ya umasikini na dhiki yenu kwa sababu ya kuwapa riziki, kama hilo lilivyokuwepo katika zama za ujinga mkubwa wenye dhaluma. Na ikiwa walikatazwa kuwaua katika hali hii ilhali ni watoto wao, basi kuwakataza kuwaua bila ya sababu au kuwaua watoto wa watu wengine ni jambo linalostahili na kufaa zaidi. "Sisi tunawaruzuku nyinyi na wao;" yaani, tumekwisha chukua dhamana ya kuwaruzuku wote. Basi si nyinyi mnaowaruzuku watoto wenu, na hata kujiruzuku nyinyi wenyewe, kwa hivyo hamna dhiki ya kuwafanyia hilo. "Wala msikaribie machafu," nayo ni madhambi makubwa na machafu "yaliyo dhahiri yake, na yaliyofichikana yake." Yaani, msiyakaribie yaliyo dhahiri yake na yaliyofichikana, au yanayohusiana na dhahiri na yanayohusiana na moyo na ndani. Na katazo la kuyakaribia machafu ni kubwa zaidi kuliko kukataza tu kuyafanya. Kwa maana hili linajumuisha kukataza vitangulizi vyake na njia zake zinazoyafikia. "Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu aliiharamisha;" nayo ni nafsi ya Kiislamu, ya kiume na ya kike, changa na nzee, njema na ovu, na ya kikafiri ambayo amekingwa kwa ahadi na agano; "isipokuwa kwa haki." Kama vile mzinifu aliyeoleka, na nafsi kwa nafsi, na mwenye kuacha dini yake na kujitenga na umma. "Hayo" yaliyotajwa "aliwausia" [Mwenyezi Mungu] "ili myatie akilini" kutoka kwa Mwenyezi Mungu wasia wake, kisha muihifadhi, kisha muizingatie, na muitekeleze. Na Aya hii iliashiria kwamba kulingana na akili ya mja, kunakuwa kusimamisha kwake kile ambacho mwenyezi Mungu alimuamrisha.