Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَا تَسُبُّوا۟ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَسُبُّوا۟ ٱللَّهَ عَدْوًۢا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ۱۰۸
{108} Mwenyezi Mungu anawakataza Waumini kufanya jambo ambalo lilikuwa linaruhusiwa, bali mwanzoni lilikuwa katika sheria. Nalo ni kuwatukana miungu wa washirikina ambao walichukuliwa kuwa viabudiwa, na miungu pamoja na Mwenyezi Mungu, ambao wanamuweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa kuidunisha na kuilaani. Lakini pindi kutukana huku kulipokuwa ni njia ya washirikina kufikia kumtukana Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye heshima yake kubwa ni lazima itakaswe kutokana na kila kasoro, na maradhi, na matusi, na kashfa; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akakataza kuwatukana miungu ya washirikina. Kwa sababu wao wanailinda dini yao na wanaitetea. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameupambia kila umma vitendo vyao ,kwa hivyo wakaviona kuwa ni vizuri, na wakavilinda na kuvizuilia kwa kila njia, mpaka wanamtukana Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye ukuu wake umethibiti katika nyoyo za walio wema na waovu, Waislamu wanaitukana miungu yao. Lakini viumbe wote marejeo yao na mwisho wao ni kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama. Watahudhurishwa kwake, na yatahudhurishwa matendo yao, kisha atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda, ya heri na maovu. Na katika Aya hii tukufu kuna ushahidi wa kanuni ya kisheria, ambayo ni kwamba njia zinazingatiwa kulingana na mambo zinayoyafikia, na kwamba njia za kilichoharamishwa - hata zikiwa zinaruhusika - zinakuwa haramu ikiwa zitafikisha katika maovu.