پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hashr
سورهٔ ۵۹

Al-Hashr

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۷

مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنْ أَهْلِ ٱلْقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ كَىْ لَا يَكُونَ دُولَةًۢ بَيْنَ ٱلْأَغْنِيَآءِ مِنكُمْ ۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمْ عَنْهُ فَٱنتَهُوا۟ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ ۷

{7} Al-Fayi ni kulingana na istilahi ya mafaqihi ni kile kilichochukuliwa kutoka kwenye mali za makafiri kwa haki, bila ya kupigana vita. Kama mali hizi walizokimbia na kuziacha kwa kuwaogopa Waislamu. Nazo ziliitwa Al-Fayi kwa sababu ilirejea kutoka kwa makafiri ambao hawakuistahiki na kuwaendea Waislamu ambao wana haki nyingi humo. Na hukumu yake kwa ujumla ni kama alivyoitaja Mwenyezi Mungu pale aliposema: “Mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji” kwa ujumla, sawa iwe ni katika zama za Mtume au baada yake kwa wale watakaoshika uongozi katika umma wake baada yake, “ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri.” Na Aya hii inafanana na Aya iliyomo katika Surat Al-Anfal, nayo ni kauli yake: “Na jueni ya kwamba ngawira mnayoipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri.” Ngawira hii inagawanywa katika sehemu tano: kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo itatumika kwa masilahi ya jumla ya Waislamu. Na humusi kwa ajili ya jamaa zake, yaani Banu Hashim na Banu Al-Muttalib, popote watakapokuwa, wanaume na wanawake wao wako sawa katika hilo. Hao Banu Al-Muttalib walijumuishwa katika humusi hii pamoja na Banu Hashim ilhali haawakuingizwa Banu Abd Manaf wengineo, kwa sababu walishiriki pamoja na Banu Hashim katika kuingia kwao katika bonde wakati Maquraishi walipofanya makubaliano ya kuwatenga na kuwafanyia uadui, kwa hivyo wakamuunga mkono Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – tofauti na wengineo, na ndiyo maana Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alisema kuhusu Banu Abdul Muttalib: “Hakika, wao hawakujitenga mbali nami wakati wa kabla ya Uislamu wala katika Uislamu.” Na humusi nyingine kwa ajili ya mayatima masikini, ambao ni wale wasio na baba na hawajabaleghe. Na humusi nyingine kwa ajili ya maskini. Na humusi nyingine kwa ajili ya wasafiri, ambao ni wageni waliokwama katika maeneo yaliyo mbali na nchi zao. Mwenyezi Mungu aliweka viwango hivi na akafanya Al-Fayi (ngawira) kuwa ni ya watu hawa maalumu, ili "isiwe ikizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu” sababu kama Mwenyezi Mungu hakupanga hivyo, basi matajiri wenye nguvu ndio wengeichukua peke yao, na wasio na uwezo hawangepata chochote kwayo, jambo ambalo lingeleta uharibifu mkubwa asioujua isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Kama vile kwa kufuata amri ya Mweneyezi Mungu na sheria yake kuna manufaa mengi yasiyo na mipaka. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaamuru kanuni na msingi wa jumla, akasema: “Na anachokupeni Mtume, kichukueni. Na anachokukatazeni, jiepusheni nacho.” Hili linajumuisha misingi ya dini na matawi yake, ya dhahiri na ya siri, na kwamba yale aliyokuja nayo Mtume inawalazimu waja kuyachukua na kuyafuata, na si halali kwenda kinyume naye, na kwamba amri ya Mtume juu ya kitu fulani, ni kama amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakuna anayepewa ruhusa wala udhuru wa kuacha amri ya Mtume, na wala hairuhusiwi kutanguliza kauli ya mtu yeyote mbele ya kauli ya Mtume. Kisha Mwenyezi Mungu akaamuru afanyiwe ucha Mungu, ambao kwa huo vinasimama imara mioyo, roho, dunia na akhera, na kwa huo mtu anapata furaha ya kudumu na ushindi mkubwa. Na kwa kuuacha, mtu anaingia katika taabu ya milele na adhabu isiyoisha. Amesema Mtukufu: “Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu” mwenye kuacha kumcha na akapendelea kufuata matamanio.