Al-Hashr
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
كَمَثَلِ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ۖ ذَاقُوا۟ وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ۱۵
{15} “Ni kama mfano wa wale waliokuwa kabla yao hivi karibuni” Hao ni makafiri wa Maquraishi ambao " Shetani alipowapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipoonana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Hakika mimi si pamoja nanyi. Hakika mimi ninaona msiyoyaona." Basi nafsi zao zikawadanganya, na wale waliowahadaa pia wakawahadaa, ambao hawakuwanufaisha kitu na hawakuwazuilia adhabu, mpaka walipofika Badr kwa kujifahiri kwao na kiburi chao, wakidhania kuwa wao watafikia matajario yao dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini. Basi Mwenyezi Mungu akampa ushindi Mtume wake na Waumini dhidi yao, na wakawaua wakuu wao na vigogo wao, na wakawateka wale waliowateka miongoni mwao, na wakakimbia wale waliokimbia, na wakaonja kwa hilo uovu huo mambo yao na matokeo ya ushirikina wao na kuvuka kwao mipaka. Haya ni katika dunia, na Akhera watapata adhabu ya Moto.