پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qamar
سورهٔ ۵۴

Al-Qamar

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۷

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ۱۷

{17} "Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka?” Yaani, hakika tumeifanya Qur-ani hii Tukufu kuwa nyepesi na rahisi katika maneno yake kwa ajili ya kuihifadhi akilini, kuitekeleza, na kufanya maana zake rahisi kwa ajili ya kuzifahamu na kuzijua vyema. Kwa sababu ndiyo mazungumzo yenye matamshi bora zaidi, na yenye maana ya ukweli zaidi, na yenye maelezo yaliyo wazi zaidi. Kwa hivyo, kila mwenye kuichukua, Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi mno katika matakwa yake, na huifanya kuwa rahisi kwake. Na ukumbusho unajumuisha kila wanachokikumbuka wanaojua kama vile halali, haramu, hukumu za maamrisho na makatazo, hukumu za kimalipo, mawaidha, mazingatio, itikadi zenye manufaa na habari za ukweli. Ndiyo maana ikawa elimu ya Qur-ani sawa iwe ni kuhifadhi moyoni na kuifasiri ndiyo elimu nyepesi zaidi na tukufu zaidi kuliko zote. Nayo ndiyo elimu yenye manufaa ambayo mtu akiitafuta mja akiitafuta, husaidiwa na Mwenyezi Mungu juu yake. Baadhi ya wema waliotangulia walisema kuhusiana na Aya hii kwamba inamaanisha: ‘Je, yuko yeyote anayetafuta elimu ili asaidiwe juu yake?’ Ndiyo maana Mwenyezi Mungu anawaita waja wake kuichukua na kuikumbuka katika kauli yake: "Lakini yupo anayekumbuka?"