پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qamar
سورهٔ ۵۴

Al-Qamar

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۴

تَجْرِى بِأَعْيُنِنَا جَزَآءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ ۱۴

{14} "Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu." Yaani, ilikuwa inakwenda na Nuhu pamoja na wale walioamini, na alivyovibeba miongoni mwa sampuli za viumbe, kwa utunzaji na ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kuzama majini. Naye ndiye Mlinzi na Mtegemewa bora. "Yawe ni malipo kwa anayekufuru." Yaani, tulimfanyia Nuhu yale tuliyofanya ya kumwokoa kutokana na kuzama majini kwa ujumla ili yawe ni malipo kwake. Kwa vile watu wake walivyomkadhibisha na kumkufuru, naye akawa na subira katika kuwalingania, na akaendelea kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, na hakuna cha kumrudisha nyuma kilichomrudisha nyuma, wala cha kumzuilia kilichomzuia kufanya hivyo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya nyingine: "Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe..." hadi mwisho wa Aya. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba tuliwaangamiza watu wa Nuhu na tukawafanyia yale tuliyowafanyia ya adhabu na fedheha ili yawe ni malipo ya ukafiri wao na ukaidi wao. Maana hii inakuwa wazi kwa yule anayesoma kwa kutia Fat-ha kwenye herufi Kaf.