Qaaf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ۖ فَذَكِّرْ بِٱلْقُرْءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ ۴۵
{45} "Sisi tunajua kabisa wayasemayo" wakikuambia miongoni mwa mambo ya kukuhuzunisha ya kukuudhi. Na ikiwa tunajua kabisa hayo, basi hakika umeshajua jinsi tunavyokutunza, na kukurahisishia mambo yako, na kukupa ushindi dhidi ya adui zako. Hebu moyo wako ufurahi, na nafsi yako itulie, na jua kwamba tunakurehemu zaidi na tunakufanyia upole sana hata kuliko unavyojifanyia mwenyewe. Kwa hivyo, hakuna unachobakisha isipokuwa kusubiri ahadi ya Mwenyezi Mungu na kufuata mfano wa wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu. "Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari." Na pia alisema: "Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoza." Na ndiyo maana akasema: "Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeiogopa ahadi ya adhabu." Na kukumbusha huko kunahusiana na yale yaliyothibiti katika akili na maumbile asili ya kupenda heri, kuipendelea na kuifanya, na kuuchukia uovu na kujiepusha nao. Lakini anakumbuka tu kwa ukumbusho yule anayeogopa onyo. Ama yule ambaye haogopi ahadi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu wala hata hakuiamini, basi huyu faida ya kumkumbusha ni kumsimamishia tu hoja ili asije sema: 'Hatukujiwa na mbashiri wala mwonyaji.'
Mwisho wa tafsiri ya Surat Qaf. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, mwanzoni, mwishoni, nje kwa hadharani na kwa siri.