Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكُمْ وَٱلْكُفَّارَ أَوْلِيَآءَ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۵۷ وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ ٱتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ۵۸
{57 - 58} Anawakataza waja wake Waumini kuwafanya Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Manasara na makafiri wengine wote kuwa marafiki wandani, kwa kuwapenda na kuwafanya marafiki wandani. Na wanawafunulia siri za Waumini, na wanawasaidia katika baadhi ya mambo yao ambayo yanaudhuru Uislamu na Waislamu. Na kwamba imani yake waliyo nayo inawawajibishia kuacha kuwafanya kuwa marafiki wandani, na inawahimiza kuwafanyia uadui. Na vile vile kushikamana kwao na kumcha Mwenyezi Mungu, ambako ni kutii amri zake na kujiepusha na makemeo yake ambayo yanawatia kwenye kuwafanyia uadui. Na vile vile yale ambayo wanayafanya washirikina na makafiri wanaowahalifu Waislamu ya kuikashifu Dini ya Waislamu na kuichukulia kama mzaha na mchezo na kuidharau na kuidunisha. Hasa Swala, ambayo ndiyo alama ya Waislamu iliyo dhahiri zaidi na ibada yao iliyo tukufu zaidi. Wao wanapoita kwa ajili yake, wanaichukulia kuwa mzaha na mchezo. Na hilo ni kwa sababu ya kutokuwa kwao na akili na ujinga wao mkubwa. Vinginevyo, lau wangekuwa na akili, wangeliinyenyekea, na wangelijua kwamba ni kubwa zaidi kuliko fadhila zote ambazo nafsi zinasifika kwazo. Kwa hivyo, mnapokwisha jua Enyi Waumini hali ya makafiri na ukubwa wa uadui wao kwenu na dini yenu; basi ambaye hatawafanyia uadui baada ya haya; itaashiria kwamba Uislamu kwake ni rahisi, na kwamba hajali mwenye kuikashifu au mwenye kukashifu kwa ukafiri na upotovu; na kwamba yeye hana kitu katika uungwana wala ubinadamu. Basi vipi unaweza kujidai kuwa una dini yenye thamani, na kwamba ndiyo dini ya haki, na nyinginezo zote ni batili, na unamridhia mwenye kuifanya kuwa mzaha na mchezo; na akaifanyia masihara hiyo na watu wake miongoni mwa watu wa ujinga na upumbavu? Basi hili ndani yake lina uchochezi juu ya kuwafanyia uadui ambao unajulikana hata kwa kila mtu ambaye ana ufahamu mdogo zaidi.