Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُحِلُّوا۟ شَعَـٰٓئِرَ ٱللَّهِ وَلَا ٱلشَّهْرَ ٱلْحَرَامَ وَلَا ٱلْهَدْىَ وَلَا ٱلْقَلَـٰٓئِدَ وَلَآ ءَآمِّينَ ٱلْبَيْتَ ٱلْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَٰنًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَٱصْطَادُوا۟ ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَـَٔانُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا۟ ۘ وَتَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلْبِرِّ وَٱلتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ ۲
{2}Yeye Mtukufu anasema: "Enyi mlioamini! Msivunje heshima ya alama za Dini za Mwenyezi Mungu." Yaani, yale aliyoharamisha ambayo aliwaamrisha kuyaheshimu na kutoyafanya. Basi kukataza huku kunajumuisha kukataza kuyafanya na kukataza kuitakidi uhalali wake, basi kunajumuisha kukataza kufanya mabaya, na kuyaitakidi. Na inaingia katika hilo kukataza yale yaliyoharamishwa katika hali ya Ihram, inaingia katika hilo yale aliyoyataja hasa kwa kauli yake. "Wala mwezi mtakatifu," yaani msiuvunje kwa kupigana vita ndani yake au mengineyo miongoni mwa aina za dhuluma. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili Katika cha Mwenyezi Mungu tangu alipoziumba mbingu na ardhi. Katika hiyo kuna minne mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Kwa hivyo, msizidhulumu nafsi zenu humo." Na wanachuoni walio wengi wanaona kuwa kupigana vita katika miezi mitakatifu kulibatilishwa kwa kauli yake Yeye Mtukufu. "Na ikiisha miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote mwakutapo." Na aya nyinginezo zenye ujumla wa amri ya kupigana vita na makafiri kabisa, na ahadi ya adhabu kwa mwenye kusalia nyuma ya kupigana vita nao kabisa. Na kwamba Nabii -rehema na amani zimshukie – alipigana na watu wa Taif katika Dhil-Qa’da, na ilhali ni katika miezi mitakatifu. Nao Wengine wakasema: hakika, Katazo la kupigana vita katika miezi mitakatifu halikufutwa kwa Aya hii na nyinginezo zilizo na katazo la hilo hususan. Na wakafasiri maandiko ambayo hayakufungiwa yaliyokuja kuhusiana na hilo na wakasema: Maandiko ambayo hayakufungiwa yanaelewekeka kwa mujibu wa yale yaliyofungiwa. Nao baadhi yao wakafafanua kwa kina na wakasema: Hairuhusiki kuanza kupigana vita katika miezi mitakatifu, lakini inaruhusika kuviendeleza na kuvikamilisha ikiwa vilianza katika miezi mingine. Na walikufasiri kupigana vita kwa Nabii -rehema na Amani zimshukie - na watu wa Taif hivyo. Kwa sababu mwanzo wa kupigana kwao kulianza huko Hunayn katika Shawwal. Na yote haya ni katika kupigana vita ambako makusudio yake siyo kujilinda. Na ama kupigana vita kwa ajili ya kujilinda ikiwa makafiri wa Kiislamu wataanzisha kupigana vita, basi hilo linaruhusika kwa Waislamu kupigana vita ili kujilinda katika mwezi mtakatifu na mingineyo kwa Ijmaa (makubaliano) ya wanachuoni. Na kauli yake, "Wala wanyama wanaopelekwa Makka kama zawadi na wale wanaofungwa vigwe kuchinjwa," yaani, wala msihalalishe wanyama wa zawadi wanaoletwa kama zawadi kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu wakati wa Hijja, au Umra, au yasiyokuwa hayo miongoni mwa wanyama wa kufugwa na wengineo. Na wala msimzuie kufika pahali pake, msimchukue kwa wizi au vinginevyo, na wala msimpuuze au kumbebesha zaidi ya uwezo wake kwa kuogopa kuharibika kwake kabla ya kupafikia pahali pake. Bali mheshimuni na mumheshimu yule aliyekuja naye. "Wala vigwe vyao." Na huyu ni aina maalum katika aina za wanyama wa dhabihu. Naye ni mnyama wa dhabihu ambaye husokotewa vigwe au misokoto na kuwekwa kwenye shingo zao, ili kudhihirisha alama za Mwenyezi Mungu. Na ili kuwahimiza watu kufuata mkondo huo, na kuwafundisha Sunnah, na ili ajulikane kuwa ni mnyama wa dhabihu ili aheshimiwe. Na kwa sababu hii kukawa kuwafunga wanyama wa dhabihu vigwe wanaopelekwa Makkah kama zawadi ni katika Sunnah na alama za kidini za Sunnah. "Wala wale wanaoelekea kuiendea Nyumba Takatifu," yaani, wale wanaoikusudia; "wakitafuta fadhila kutoka kwa Mola wao Mlezi na radhi." Yaani, mwenye kuikusudia Nyumba hii tukufu, hali ya kuwa amekusudia fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya biashara na mapato yanayoruhusiwa, au makusudio yake ni radhi za Mwenyezi Mungu kwa njia kuiendea kwa ajili ya Hijja yake, na Umra, na kuizunguka, na swala, na aina nyinginezo za ibada; basi msimkabili kwa ubaya wala msimdunishe. Bali mkiwaheshimu na muwape heshima wageni wanaozuru Nyumba ya Mola wako Mlezi. Imejumuishwa katika jambo hili ni amri ya kuzilinda njia zinazoelekea kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na kuwafanya waiendeao wawe na utulivu na utulivu, wasiogope kuua au kupungukiwa chochote, wala mali yao kutokana na kodi za haramu, na kunyang'anywa na mfano wa hayo. Na Aya hii tukufu imefanywa kuwa mahususi kwa kauli yake Yeye Mtukufu. "Enyi mlioamini! Hakika, washirikina ni najsi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu." Basi Mshirikina hafai kuwezeshwa kuingia kwenye eneo takatifu. Na katazo mahususi katika Aya hii la kumkabili mwenye kuikusudia Nyumba hali ya kuwa anatafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu au radhi zake inaonyesha kuwa mwenye kuikusudia ili kufanya upotofu humo kwa maasia. Basi katika ukamilifu wa kulitukuza eneo takatifu ni kumzuia yule ambaye hali yake ni nii, ili asifanye ufisadi katika Nyumba ya Mwenyzi Mungu. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema, "Na mwenye kutaka kufanya upotofu humo kwa dhuluma, basi tutamwonjesha adhabu chungu." Na alipowakataza kuwinda katika hali ya Ihram, akasema, "Na mkishatoka katika Ihram, basi windeni. yaani, mnapotoka katika hali ya Ihram ya Hijja au Umra, [na mkatoka nje ya eneo takatifu]. Basi inakuwa halali kwenu kuwinda, na kunaisha kuharamisha huko. Na amri baada ya katazo inarudisha mambo katika hali yake ya hapo awali. "Wala kuwachukia watu kwa kuwa waliwazuia kuufikia Msikiti mtakatifu kusiwapelekeeni kupita mipaka." Yaani, isiwabebe chuki juu ya watu, na uadui wao na kupita kwao mipaka kwenu, kwani waliwazuia kuufikia Msikiti ili nanyi muwapindukie mipaka mkitafuta kupona kutoka kwao. Kwa maana, inamlazimu mja kushikamana na amri ya Mwenyezi Mungu na achukue njia ya uadilifu, hata akifanyiwa kosa, au kudhulumiwa, au kupindukiwa mipaka. Kwa hivyo haruhusiwi kusema uongo juu ya yule waliyemdanganyishia au kumsaliti yule aliyemsaliti. "Na saidianeni katika wema na uchamungu," yaani na msaidiane nyinyi kwa nyinyi juu ya wema. Nalo ni jina linalojumuisha kila analolipenda Mwenyezi Mungu, miongoni mwa matendo ya dhahiri na ya ndani katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za wanadamu. Na uchamungu katika pahali hapa ni jina linalojumuisha kuacha yote anayoyachukia Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwa matendo ya dhahiri na ya ndani. Na kila sifa miongoni mwa sifa za heri iliyoamrishwa kufanywa au sifa miongoni mwa sifa za uovu ulioamrishwa kuachwa. Kwa maana mja ameamrishwa kuyafanya yeye mwenyewe, na kwa msaada wa wengine miongoni mwa ndugu zake Waumini kwa kila kauli imfanyayo mtu kuyaanza, na imtiyayo ukakamavu juu yake, na kwa kila kitendo pia. "Wala msisaidiane katika dhambi," nayo ni kuyafanyia maasia ujasiri ambayo mwenyewe anapata dhambi na anachukuliwa kosa "na kupita mipaka." Nako ni kukiuka mipaka ya viumbe katika damu zao, na mali zao, na heshima zao. Basi ni lazima juu ya mja mwenyewe kujizuia kutokana na kila maasia na dhuluma, kisha awasaidie wengine juu ya kuyaacha. "Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu," juu ya mwenye kumuasi, na akajasiri kufanya yale aliyoharamisha. Basi jihadharini na maharamisho; ili isije ikawafika adhabu yake ya sasa na ya baadaye.