پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zukhruf
سورهٔ ۴۳

Az-Zukhruf

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۳۲

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَـٰتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ۳۲

{32} Mwenyezi Mungu akasema akipinga pendekezo lao hilo: "Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako Mlezi?" Yaani, kwani wao ndio wanaozihifadhi rehema za Mwenyezi Mungu, na kwamba kuziendesha kwake kuko mikono mwao, ndiyo wakampa unabii na ujumbe wamtakaye, na wakamzuilia wamtakaye? "Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi" Yaani, katika maisha ya dunia, "na" hali ni kwamba rehema "za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya" ya kidunia. Kwa hivyo, ikiwa maisha ya waja na riziki zao za kidunia ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Yeye ndiye anayezigawanya miongoni mwa waja wake, kwa hivyo humkunjulia riziki amtakaye na kumkunjia amtakaye kwa hekima yake. Basi rehema yake ya kidini - ambayo ya juu yake kabisa ni unabii na ujumbe - inafaa zaidi na zaidi kuwa mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi kuliko wote ni wapi anaweka ujumbe wake. Basi ikajulikana kuwa pendekezo lao hilo ni batili, na kwamba uendeshaji wa mambo yote, ya kidini na ya kidunia, uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake. Huku ni kuwashawishi kuhusiana na kukosea kwao katika pendekezo lao hilo ambalo hawana chochote mikononi mwao kuhusiana nalo. Hilo si ila ni dhuluma tu na kukataa haki. Na kauli yao, "Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii" Lau wangelijua uhakika wa watu na sifa zinazojulikana kwazo utukufu wa mtu, na ukubwa wa hadhi yake kwa Mwenyezi Mungu na kwa viumbe vyake, wangejua kwamba Muhammad bin Abdullah bin Abdul-Muttalib ndiye mtu mkubwa zaidi kuliko watu wote kwa hadhi, wa juu wao zaidi kwa fahari, mkamilifu wao zaidi wa akili, mwenye elimu zaidi yao wote, mwenye rai bora zaidi, dhamira na uamuzi mzuri, mkamilifu wao zaidi wa tabia, mpana wao zaidi wa rehema, mwenye huruma zaidi yao wote, mwongofu zaidi yao wote, na mchamungu zaidi yao. Yeye ndiye nguzo ya duara la ukamilifu, na kwake ndiko zinaishia sifa za ukamilifu za wanadamu. Tambueni! Yeye ndiye mwanamume wa ulimwengu wote, ambaye wanajua hilo marafiki zake na maadui zake. Isipokuwa wale waliopotea na wenye kutakabari. Basi vipi washirikina watampendelea zaidi yake mtu ambaye hata hatawahi kunusa chembe ya ukamilifu ya uzito wa chungu, na ambaye dhamiria yake na mwisho wa akili yake ni kumfanya sanamu au mti kuwa ndiye mungu wake ambaye anayemuabudu, kumwomba na kujikurubisha kwake au jiwe lisilomdhuru wala kumnufaisha, wala halipeani wala halinyimi, nalo ni mzigo kwa bwana wake, ambalo linahitaji mtu wa kumfikishia masilahi yake? Je, haya si chochote ila ni matendo ya wapumbavu na wendawazimu? Mtu kama huyu anawezaje kufanywa kuwa mkuu? Au vipi atafanywa kuwa bora kuliko mwisho wa Mitume na bwana wa wana wa Adam – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake? Lakini wale waliokufuru hawatumii vyema akili zao. Katika aya hii, kuna tanabahisho juu ya hekima ya Mwenyezi Mungu katika kuwaboresha baadhi ya waja kuliko wengine katika ulimwengu huu; "ili baadhi yao wawafanye wenginewe wawatumikie" katika kazi, ufundi na sanaa mbalimbali. Lau kuwa watu wote wangekuwa sawa katika utajiri, basi hawangehitajiana, na masilahi na manufaa yao mengi yangevurugika. Aya hii pia ina ushahidi kwamba neema zake za kidini ni bora kuliko neema zake za kidunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya nyingine, "Sema: 'Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.'"