Al-Ghaafir
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَٱصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَٱسْتَغْفِرْ لِذَنۢبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِٱلْعَشِىِّ وَٱلْإِبْكَـٰرِ ۵۵
{55} "Basi subiri" ewe Mtume, kama walivyosubiri wale waliokuwa kabla yako miongoni mwa Mitume wenye stahamala kubwa. "Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli." Haina shaka yoyote, wala si ya uongo kiasi kwamba inakuwa vigumu kwako kuwa na subira. Bali ni haki iliyo safi kabisa na uwongofu safi ambao wenye subira husubiri juu yake, na watu wenye uhafamu mkubwa hujitahidi kushikamana nayo. Kwa hivyo, kauli yake: "Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli" ni katika visababu vinavyohimiza juu ya kuwa na subira katika kumtii Mwenyezi Mungu na kujiepusha na anayoyachukia. "Na omba msamaha kwa dhambi zako" zinazokuzuia kufuzu na kufikia furaha yako. Basi hapa akawa amemuamrisha kuwa na subira ambamo kunapatikana yale anayopenda mtu, na akamuamrisha pia aombe maghfira ambayo ndani yake kuna kuzuia yote yanayotahadhariwa, na akamuamrisha kumtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumsifu, hasa "jioni na asubuhi" ambao ndio wakati bora, na ndani yake kuna mambo mbalimbali ya wajibu na yale yanayopendekezwa, kwa sababu hayo yanasaidia juu ya mambo yote.