Al-Ghaafir
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالُوٓا۟ أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ۖ قَالُوا۟ بَلَىٰ ۚ قَالُوا۟ فَٱدْعُوا۟ ۗ وَمَا دُعَـٰٓؤُا۟ ٱلْكَـٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ ۵۰
{50} Kisha "watasema" wakiwakaripia na wakiwabainishia kuwa uombezi wao huo hautowanufaisha kitu wala dua yao hiyo haitowafaa chochote: "Je, hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilizo wazi," ambazo kwazo mliweza kuijua haki na njia iliyonyooka, na yale yanayomuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu na yale yanayomuweka mbali zaidi? "Watasema: Kwani," walitujia na hoja zilizowazi, kwa hivyo hoja ya Mwenyezi Mungu ya uhakika ikasimama juu yetu, lakini tukafanya dhuluma na tukaikaidi haki baada ya kudhihirika kwake. "Watasema" walinzi hao wa Motoni wakiwaambia watu wa Motoni, huku wakijitenga mbali na suala la kuwaombea dua na kuwafanyia uombezi. "Basi ombeni" wenyewe, lakini je, dua hii ina manufaa yoyote au la? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure." Kwa sababu ukafiri huharibu matendo yote na unazuia kukubaliwa dua.