پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورهٔ ۴

An-Nisaa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۸۸–۸۹

فَمَا لَكُمْ فِى ٱلْمُنَـٰفِقِينَ فِئَتَيْنِ وَٱللَّهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوٓا۟ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا۟ مَنْ أَضَلَّ ٱللَّهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلًا ۸۸ وَدُّوا۟ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُوا۟ فَتَكُونُونَ سَوَآءً ۖ فَلَا تَتَّخِذُوا۟ مِنْهُمْ أَوْلِيَآءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَخُذُوهُمْ وَٱقْتُلُوهُمْ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ ۖ وَلَا تَتَّخِذُوا۟ مِنْهُمْ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ۸۹

{88 - 89} Wanafiki waliokusudiwa waliotajwa katika Aya hizi ni wale wanafiki walioudhihirisha Uislamu wao na hawakuhama licha ya ukafiri wao. Na palikuwa na mchanganyiko juu yao miongoni mwa maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi. Basi baadhi yao waliona ugumu katika kupigana vita nao, na kukataa kufanya urafiki wandani nao kwa sababu ya kile walichodhihirisha cha imani, na baadhi yao walijua hali zao kutokana na ushahidi wa matendo yao na wakahukumu kuwa wao ni makafiri. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawajulisha kwamba hawapaswi kuwa na mchanganyiko kuhusiana nao, na wala msishuku. Bali jambo lao liko wazi na halina tatizo. Wao kwa hakika ni wanafiki, na ukafiri wao umerudia na wakapenda pamoja na hilo kwamba mkufuru nyinyi, na kwamba muwe mfano wao. Kwa hivyo, mkishahakikisha hilo kwao, “Basi, msifanye marafiki wandani miongoni mwao.” Na haya yanalazimu kutowapenda, kwa sababu, urafiki wandani ni tawi la upendo. Na inalazimu pia kuwachukia na kuwa na uadui nao. Kwa sababu, kukataza kitu ni amri ya kinyume chake. Na jambo hili limepewa muda hadi kuhama kwao. Hivyo basi, wakihama, wanafanyiwa yale ambayo Waislamu wanafanyiwa, kame vile Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alivyokuwa akiwatekelezea hukumu za Uislamu kwa kila aliyekuwa pamoja naye na akahamia kwake, sawa alikuwa ni Muumini wa kweli au mwenye imani ya dhahiri tu. Na kwamba ikiwa hawatahama na wakajitenga na kuhama, “basi wakamateni, na waueni popote mnapowapata.” Yani katika wakati wowote na pahali popote. Na hili ni miongoni mwa ushahidi wenye kuashiria kuwa uharamu wa kupigana vita katika miezi mitukufu kulibatilishwa, kama ilivyo kauli ya wengi wa wanachuoni. Lakini, wale wanaopinga hilo wanasema, “Haya ni maandiko ambayo hayakufungiwa ambayo yanapswa kueleweka kulingana na kule kufungia, kuliko katika uharamisho wa kupigana vita katika miezi mitukufu.