An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
مَّآ أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ ٱللَّهِ ۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَـٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا ۷۹
{79} Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Yaliyokupata katika mazuri” yani katika Dini na dunia, “basi ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Yeye ndiye aliyeyaneemesha, na akayafanya kuwa mepesi kwa kusahihisha sababu zake. “Yaliyokusibu katika mabaya” katika Dini na dunia “basi ni kutoka kwako mwenyewe.” Yani kwa sababu ya dhambi zako, na kuchuma kwako, na yale anayosamehe Mwenyezi Mungu ni mengi zaidi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwafungulia waja wake milango ya fadhili zake, na akawaamrisha kuingia kwa sababu ya wema wake na fadhila zake. Na akawajulisha kuwa maasia yanazuia fadhila zake. Kwa hivyo, mja akiyafanya, basi kamwe asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe. Kwa maana, yeye mwenyewe ndiye aliyejizuia kuzifikia fadhila za Mwenyezi Mungu na wema wake. Kisha akajulisha kuhusu ujumla wa ujumbe wa Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - Akasema, “Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi” kwamba wewe kwa hakika, ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa yale aliyokuunga mkono kwayo ya nusura yake, na miujiza ing'aayo na hoja zilizo wazi. Basi ndiyo ushahidi mkubwa zaidi kuliko zote, kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Sema: Ni kitu gani chenye ushahidi mkubwa zaidi? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi.” Basi, ikijulikana kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu kamili, Mwenye uwezo timilifu, Mwenye hekima kubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu alimuunga mkono Mtume wake kwa yale aliyomuunga mkono kwayo, na akamnusuru nusura mkubwa; basi kunakuwa na yakini kwa sababu ya hayo kwamba yeye hakika ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Vinginevyo, ikiwa lau kuwa angelimzulia baadhi ya maneno, basi bila ya shaka angelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika angelimkata mshipa mkubwa wa moyo!