An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ ءَامِنُوا۟ بِمَا نَزَّلْنَا مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبْلِ أَن نَّطْمِسَ وُجُوهًا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدْبَارِهَآ أَوْ نَلْعَنَهُمْ كَمَا لَعَنَّآ أَصْحَـٰبَ ٱلسَّبْتِ ۚ وَكَانَ أَمْرُ ٱللَّهِ مَفْعُولًا ۴۷
Yeye Mtukufu anawaamrisha Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Manasara wamwamini Mtume Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - Na katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyateremshia katika Qur-ani Tukufu, na kigezo cha vinginevyo miongoni mwa vitabu vilivyotangulia ambacho kilivisadikisha. Kwani vilijulisha kukihusu, na kilipotokea kile kilichojulishwa, kikawa kimesadikisha habari hiyo. Na pia, ikiwa hawaiamini Qur-ani hii, basi hawajaamini yale yaliyo katika mikono yao miongoni mwa vitabu. Kwa sababu vitabu vya Mwenyezi Mungu vinasadikishana vyenyewe kwa vyenyewe na vinaafikiana vyenyewe kwa vyenyewe. Kwa hivyo madai ya kuamini baadhi yake bila ya vingine ni madai batili, hayawezi kuwa ya kweli. Na katika kauli yake, "Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo" kuna kuwahimiza. Na kwamba inafaa waifanyie haraka mbele ya watu wengine kwa sababu ya yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa elimu na Kitabu kitu kinacholazimu kwamba hali yao iwe kubwa kuliko ya wengineo. Na kwa sababu ya hayo, akawaahidi adhabu juu ya kutoamini. Akasema, "Kabla hatujazifutilia mbali nyuso tukazipeleka nyuma yake." Na haya ni malipo ya aina sawa na yale waliyokuwa wakiyatenda. Kama walivyoiacha haki na wakaipendelea batili, na wakaugeuza uhakika, kwa hivyo wakaifanya batili kuwa haki, na haki kuwa batili, wakalipwa kwa aina sawa na hayo kwa kufutiliwa mbali nyuso zao kama walivyofutilia mbali haki. Na kuzirudisha kwake nyuma yake ni kuziweka kwenye visogo vyao. Na hili ndilo jambo baya zaidi linaloweza kuwa. "Au tuwalaani kama tulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi)," kwa kuwafukuza kutoka katika rehema yake na kuwaadhibu kwa kuwafanya manyani, kama alivyowafanya ndugu zao ambao walikiuka mipaka kuhusiana na (siku ya) Sabato. Na tukawaambia: Kuweni manyani, mliodhalilika. "Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike." Kama kauli yake, "Hakika, amri yake anapotaka kitu ni akiambie tu: Kuwa! Na kinakuwa."