An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ۲۶
{26} Yeye Mtukufu anajulisha neema yake kubwa, na kipawa chake kikubwa, na malezi yake mazuri kwa waja wake Waumini, na wepesi wa dini yake, akasema, “Mwenyezi Mungu anataka kwamba awabainishie” Yani, yote mnayohitaji kubainishiwa miongoni mwa haki na batili, na halali na haramu. “Na awaongoze nyendo za wale waliokuwa kabla yenu.” Yani, wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaaneemesha miongoni mwa Mitume na wafuasi wao katika mienendo yao yenye kusifiwa, na matendo yao ya sawasawa, na sifa zao kamili, na kuwezeshwa kwao kukamilifu. Basi kwa sababu ya hayo, akatekeleza alilotaka, na akawawekea wazi, na akabainisha kwa uwazi kama alivyowabainishia wale waliokuwa kabla yenu, na akawaongoza uwongofu mkubwa katika elimu na matendo. “Na akubali toba zenu;” yani, awafanyie upole katika hali zenu, na yale aliyowawekea kama sheria, ili muweze kusimamia juu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwawekea mipaka. Na kutosheka na yale aliyoyahalalisha, ndiyo dhambi zenu zipunguke kwa sababu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwarahisishia. Na kwa sababu ya hayo, katika kukubali kwake toba ya waja wake, na katika kukubali toba yao ni kwamba wanapotenda dhambi, anawafungulia milango ya rehema, na akaziwezesha nyoyo zao kumrudia Yeye, na kunyenyekea mbele yake, kisha anawakubalia toba kwa kuyakubali yale aliyowawezesha. Basi Sifa njema ni zake na shukurani kwa hayo. Na kauli yake, “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.” Yani, [ni Mwenye elimu kamili], mwenye hekima kamili. Basi katika elimu yake ni kwamba aliwafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. Na miongoni mwake ni mambo haya na mipaka. Na katika hekima yake ni kwamba anamkubalia toba yule ambaye hekima yake na rehema zake zinahitaji kwamba akubaliwe toba. Na anamwacha yule ambaye hekima yake na uadilifu wake vinahitaji kwamba hastahili kukubaliwa toba.