An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَءَاتُوا۟ ٱلْيَتَـٰمَىٰٓ أَمْوَٰلَهُمْ ۖ وَلَا تَتَبَدَّلُوا۟ ٱلْخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِ ۖ وَلَا تَأْكُلُوٓا۟ أَمْوَٰلَهُمْ إِلَىٰٓ أَمْوَٰلِكُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبًا كَبِيرًا ۲
Na kauli yake Yeye Mtukufu:
{2} Hili ndilo jambo la kwanza alilousia katika haki za viumbe katika sura hii. Nao ni mayatima waliofiwa na wazazi wao wanaowalea hali ya kuwa wao ni wadogo, na dhaifu, na wasioweza kujisimamia masilahi yao. Kwa hivyo, Yeye Mwingi wa huruma, Mwingi wa Rehema akawaamrisha waja wake kuwafanyia wema, na kwamba wasizikaribie mali zao isipokuwa kwa njia iliyo bora zaidi. Na kwamba wawape mali zao - wakifikia utu uzima na wakawa na uamuzi wa busara- kamili na nyingi. Na kwamba wasibadilishe viovu, ambako ni kuila mali ya yatima bila ya haki. "Kwa vizuri" ambayo ni halali ambayo haina ubaya wowote wala matokeo mabaya. "Msile mali zao pamoja na mali zenu" yani, pamoja na mali zenu. Na ndani yake kuna tahadharisho juu ya ubaya wa kula mali yao katika hali hii. Ambayo mtu amejitosheleza bila ya kuihitaji kwa sababu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa kutokana na riziki katika mali yake. Kwa hivyo, atakayefanya ujasiri wa kufanya hivyo katika hali hii; basi kwa hakika atakuwa amebeba "jukumu kubwa." Yani, dhambi kubwa na mzigo mkubwa. Na katika kubadilisha kibaya kwa kizuri ni mlezi kuchukua katika mali ya thamani ya yatima kisha anaweka badala yake kutoka kwa mali yake duni. Na ndani yake kuna ulezi juu ya mayatima. Kwa sababu linaloambatana na kumpa yatima mali yake ni kuthibiti ulezi wa mwenye kupeana juu ya mali yake yatima. Na ndani yake kuna amri ya kutengeneza mali ya yatima. Kwa sababu, ukamilifu wa kumpa mali yake ni kuilinda na kuifanyia yale yanayoifanya kuwa nzuri, na kuikuza na kutoziweka kwa yale yanayofisha na yale yaliyo hatari.