پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورهٔ ۴

An-Nisaa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۶

وَٱلَّذَانِ يَأْتِيَـٰنِهَا مِنكُمْ فَـَٔاذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا۟ عَنْهُمَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ۱۶

{16} "Na" vivyo hivyo "wawili kati yenu wafanyao hayo;" yani, machafu haya "miongoni mwenu" katika wanaume na wanawake. "Basi waudhini" kwa kauli, na kuwakemea, na kwa kipigo chenye kuzuia uchafu huu. Na kwa msingi huo, ikiwa wanaume watafanya uchafu huu, wanaudhiwa. Nao wanawake wanazuiwa na kuudhiwa. Na mwisho wa kuzuia ni kifo, nako kuudhi mwisho wake ni toba na kutengenea. Ndiyo maana akasema, "Na wakitubia;" yani, wakiiacha dhambi waliyoifanya, na wakaijutia, na wakaazimia kutoifanya tena, "na wakatengenea" kwa matendo yenye kuashiria ukweli wa toba. "Basi waacheni," yani acheni kuwaudhi. "Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu." Yani, mwenye kukubali toba kwa wingi kutoka kwa watendao dhambi, waliokosa, Mwenye rehema kubwa, na ihsani ambayo katika wema wake ni kwamba aliwaongoza kwenye toba; na akaikubali kutoka kwao, na akawasamehe kwa yale waliyoyafanya. Na inachukuliwa kutoka katika aya hizi mbili kwamba ushahidi juu ya zinaa ni [lazima] kuwepo na wanaume wanne Waumini, na katika mlango wa kile kinachostahiki zaidi na kinachofaa zaidi ni kuweka sharti kwamba wawe waadilifu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alilitilia mkazo jambo la uchafu huu kwa sababu ya kuwasitiri waja wake, kiasi kwamba hawakubaliwi katika hilo wanawake peke yao, wala pamoja mwanamume mmoja, wala chini ya wanaume wanne. Na ni lazima washuhudie waziwazi kama zilivyoashiria hilo hadithi sahihi. Na Aya hii pia inavyoashiria hivyo aliposema, "washuhudisheni watu wanne katika nyinyi," hakutosheka na hayo mpaka aliposema, "Na wakishuhudia." Yani, ni lazima kuwe kushuhudia kwa waziwazi kwa jambo ambalo linashuhudiwa kwa macho bila ya kusema kusiko kwa moja kwa moja wala tasfida. Na inachukuliwa kutoka kwake kwamba kuudhi kwa kauli, na matendo, na kuzuia Mwenyezi Mungu alikwisha viweka kama sheria ili iwe adhabu kwa aina yenyewe ya maasia ambayo kemeo linatimia kwayo.