An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَّا يُحِبُّ ٱللَّهُ ٱلْجَهْرَ بِٱلسُّوٓءِ مِنَ ٱلْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ۱۴۸
{148} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba hapendi kutajwa mabaya hadharani; yani, anachukia hilo, na anaadhibu juu yake. Na hili linajumuisha maneno yote mabaya ambayo ni mabaya na yanahuzunisha. Kama vile kutukana, kukashifu, na kadhalika. Kwani hayo yote ni katika yale yaliyokatazwa, ambayo Mwenyezi Mungu anayachukia. Na maana yake isiyo ya moja kwa moja inaonyesha kwamba anapenda usemi mzuri. Kama vile utajo wake, na maneno mazuri na ya upole. Na kauli yake, "isipokuwa kwa aliyedhulumiwa." Yaani, yeye anaruhusiwa kumuapiza yule aliyemdhulumu, na kumlalamika juu yake, na kumsema ubaya waziwazi kwa yule aliyemsema yeye kwa ubaya waziwazi bila ya kumsingizia uongo, wala kumuongezea juu ya dhuluma yake, wala asiruke mipaka kwa kumtukana mtu asiyekuwa yule aliyemdhulumu. Na licha ya hayo, kusamahe kwake na kutomlipiza ni bora zaidi. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo ujira wake yako kwa Mwenyezi Mungu." "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua." Na kwa kuwa Aya hii ilijumuisha maneno mabaya, na mazuri na yanayoruhusiwa, Yeye Mtukufu alijulisha kwamba Yeye ndiye Mwenye kusikia, hivyo anayasikia maneno yenu. Kwa hivyo, jihadharini kuzungumza jambo ambalo litamkasirisha Mola wenu Mlezi, naye awaadhibu [kwa hilo]. Na pia ndani yake kuna kuhimiza juu ya usemi mzuri. Anajua nia zenu na chanzo cha maneno yenu.