An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَآ أَمَانِىِّ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوٓءًا يُجْزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدْ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ۱۲۳
{123} Yani amri, na wokovu na utakaso "kwa matamanio yenu, wala si matamanio ya Watu wa Kitabu." Na Matamanio ni mazungumzo ya nafsi yasiyokuwa na matendo, yanayofungamana na madai matupu, ikiwa yatalinganishwa na mfano wake, yangekuwa katika jinsia yake. Na hii ni ya jumla katika kila jambo. Basi vipi kuhusu imani na furaha ya milele? Kwani matamanio ya Watu wa Kitabu Mwenyezi Mungu alikwisha julisha juu yake kwamba: “Walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao,” na wengineo miongoni mwa wale wasiofungamana na Kitabu wala Mtume, anastahiki zaidi na anafaa zaidi. Vile vile Mwenyezi Mungu aliingiza katika hilo yule anayefungamana na Uislamu kwa sababu ya ukamilifu wa uadilifu na kutenda haki. Kwa maana, kujinasibisha tu na dini yoyote ile hakufai kitu ikiwa mtu hatatoa hoja juu ya usahihi wa madai yake. Kwa hivo, Vitendo vinathibitisha madai au kuyakanusha. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Mwenye kufanya ubaya, atalipwa kwa huo," Na hili linajumuisha watenda matendo wote, kwa sababu ubaya unajumuisha dhambi yoyote ile, miongoni mwa dhambi ndogo yake au kubwa yake, na pia inajumuisha kila adhabu, chache au nyingi, ya kidunia au ya kiakhera. Na watu katika nafasi hii ni daraja mbalimbali ambazo hazijui isipokuwa Mwenyezi Mungu, miongoni mwa wenye machache, na wenye mengi. Kwa hivyo yule ambaye matendo yake yote ni mabaya, na hawi isipokuwa kafiri, anapokufa bila kutubia, atalipwa kudumu katika adhabu chungu. Na yule ambaye matendo yake ni mema, naye akawa mnyoofu katika hali zake nyingi, lakini wakati mwingine anafanya baadhi ya madhambi madogo madogo, basi yale yanayompata miongoni mwa wasiwasi, na huzuni, na madhara, na baadhi ya maumivu katika mwili wake, au moyo wake, au mpenzi wake, au mali yake, na mfano wake, basi hayo yanasitiri dhambi zake. Nayo miongoni mwa yale anayolipwa kwayo juu ya matendo yake, Mwenyezi Mungu aliyaweka kwa sababu ya upole kwa waja wake. Na kati ya hali hizi mbili, kuna daraja nyingi. Na malipo haya ya juu ya matendo mabaya ya jumla ni mahususi kwa wasiotubia. Kwa maana, mwenye kutubia dhambi, ni kama yule asiyekuwa na dhambi. Kama lilivyoashiriwa hilo na maandiko. Na kauli yake, "wala hatajipatia kando na Mwenyezi Mungu mlinzi wala wa kumnusuru," ili kuondoa baadhi ya yale ambayo huenda yakadhaniwa kuwa anayestahiki kulipwa kwa matendo yake, huenda ana rafiki mwandani au msaidizi au mwombezi ambaye atamzuia kufikiwa na yale alichostahiki. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba hilo halipo. Kwani hatakuwa na rafiki mwandani atakayempa kile anachotaka wala wa kumnusuru atakayemzuia kutokana na kinachoogopwa isipokuwa Mola wake Mlezi, na Mmiliki wake.