An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَمَن يَكْسِبْ إِثْمًا فَإِنَّمَا يَكْسِبُهُۥ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ۱۱۱
{111} Kisha akasema, “Na mwenye kuchuma dhambi, basi ameichumia nafsi yake mwenyewe.” Na hili linajumuisha kila lenye kumfanya kupata dhambi, liwe dogo au kubwa. Kwa hivyo, mwenye kuchuma baya, basi adhabu yake ya kidunia na ya kiakhera ni juu ya nafsi yake, na haivuki kwenda kwa mwingine. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, “Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe.” Lakini yakidhihiri mabaya na yasikatazwe, adhabu yake inakuwa ya jumla, na dhambi yake inakuwa yenye kujumuisha. Basi pia haitoki nje ya hukumu ya Aya hii tukufu. Kwa sababu mwenye kuacha kukataza kwa wajibu,basi atakuwa amechuma baya. Na katika hili kuna kubainisha uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hekima yake kwamba hamuadhibu yeyote kwa dhambi ya mtu yeyote, wala hamuadhibu yeyote zaidi ya adhabu iliyotokana na dhambi yake. Na ndiyo maana akasema, “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.” Yani ana elimu kamili na hekima kamili. Na katika elimu yake na hekima yake ni kwamba anaijua dhambi, na yale aliyoyafanya, na sababu iliyompelekea kuifanya, na adhabu inayotokana na kuifanya. Na anaijua hali ya mwenye dhambi kwamba, akifanya dhambi kwa sababu ya kushindwa na nguvu za utashi wa nafsi yake, yenye kuamrisha mabaya pamoja na kurudi kwake kwa Mola wake Mlezi katika nyakati zake nyingi, kwamba atamfutia dhambi, na atamwezesha kutubia, hata kama alifanya kwa ujasiri wake juu ya maharamisho kwa kudharau kwamba Mola wake Mlezi anamwona, na kughafilika na adhabu yake, basi huyu yuko mbali na kufutiwa dhambi, kuwezeshwa kutubia.