Az-Zumar
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلْأَنْعَـٰمِ ثَمَـٰنِيَةَ أَزْوَٰجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِكُمْ خَلْقًا مِّنۢ بَعْدِ خَلْقٍ فِى ظُلُمَـٰتٍ ثَلَـٰثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ ٱلْمُلْكُ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ۶
{6} Na katika nguvu zake ni kuwa: "Amewaumba kutokana na nafsi moja" pamoja na wingi wenu na kutawanywa kwenu katika ardhi." Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile" ili apate utulivu kwake, naye mke huyo pia apate utulivu kwake, na neema ikamilike kwa hayo. "Na akawaletea wanyama wa mifugo jozi nane." Kama alivyozitaja katika Surat Al-An'am: "Wawili katika kondoo na wawili katika mbuzi. Na wawili katika ngamia na wawili katika ng'ombe." Hawa aliwataja kwa njia maalumu pamoja na kwamba pia aliwateremsha wanyama wengine kwa sababu ya masilahi ya waja wake kwa sababu ya manufaa yao mengi, ujumla wa masilahi yake na heshima yake. Na kwamba wao tu ndio wanaosifika na mambo ambayo hayapo katika wengineo; kama vile dhabihu, mnyama apelekwaye Makka kama zawadi ya Msikiti Mtukufu, wanyama wachinjwao kwa ajili ya kuzaa mwana, wanyama watolewao Zakaa na wanyama watolewao kwa ajili ya fidia ya mauaji. Alipotaja kuumbwa kwa baba yetu na mama yetu, akataja mwanzo wa kuumbwa kwetu, akasema: "Anawaumba katika matumbo ya mama zenu umbo baada ya umbo," yaani, hatua baada ya hatua, ilhali mko katika hali ambayo hauwagusi mkono wa kiumbe chochote wala haliwaangalii jicho lao lolote. Naye akawalea katika sehemu hiyo finyu "katika viza vitatu;" giza la tumbo, giza la tumbo la uzazi, na giza la plasenta. "Huyu" ambaye ameziumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi,akakuumbeni na akakuumbieni wanyama wa mifugo, akakuneemesheni, "Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi" anayepaswa kufanyiwa uungu na kuabudiwa. Basi kama vile Yeye ndiye Mmoja tu katika kuumba kwake na malezi yake, bila mshirika yeyote katika hayo, basi Yeye ndiye Mmoja katika uungu wake na hana mshirika yeyote. Ndiyo maana akasema: "Hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?" Mkaanza kuabudu viabudiwa visivyo Yeye ambavyo haviendeshi chochote, na wala havina chochote katika jambo hilo, baada ya kubainishiwa kwamba Yeye tu ndiye anayestahiki kukusudiwa!