پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
سورهٔ ۳۹

Az-Zumar

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۸

ٱلَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ ٱلْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُۥٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَىٰهُمُ ٱللَّهُ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمْ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ ۱۸

{18} Na alipojulisha kwamba wana bishara njema, Mwenyezi Mungu alimwamrisha kwamba awabashirie na akataja maelezo ambayo kwayo waliistahiki bishara hiyo njema, akasema: "Basi wabashirie waja wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata lililobora yao." Haya yanajumuisha aina zote za maneno. Wao wanasikiliza yote yanayosemwa ili watofautishe kati ya kile kinachopaswa kupendelewa na kile kinachopaswa kuepukwa. Ndiyo ilikuwa ni sehemu ya azimio lao na sababu na akili ya nzuri ni kwamba wanafuata maneno bora tu, ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume Wake. Kama alivyosema katika Sura hii: "Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana..." hadi mwisho wa Aya. Kuna suala muhimu katika Aya hii, ambalo ni kwamba pale alipojulisha kuhusu watu hawa waliosifiwa kwamba wanasikiliza yanayosemwa na kufuata yaliyo bora zaidi kati yake, ni kana kwamba ilisemwa: 'Je, ipo njia ya kujua maneno hayo yaliyobora zaidi ili tuweze pia kusifika na sifa za watu wenye akili nzuri hawa, na ili tujue kwamba anayeyapendelea ni miongoni mwa watu wenye akili nzuri?' Ikasemwa: Ndiyo,yaliyobora zaidi ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: "Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana..." hadi mwisho wa Aya. Hao "ambao husikiliza maneno, wakafuata lililobora yao,hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu" kufikia maadili na vitendo bora zaidi, "na hao ndio wenye akili" safi. Katika akili yao nzuri na azimio lao ni kwamba walitambua kilicho kizuri kutokana na mengineyo yote, na wakapendelea yale yafaayo kuliko mengine yote, na hii ni alama ya kwamba wana akili nzuri,wala hakuna alama ya kuwa na akili nzuri kuliko hii. Kwani yule asiyeweza kutofautisha kati ya maneno mazuri na mabaya si katika watu wenye akili nzuri, au mwenye kuyatofautisha lakini matamanio yake yaliishinda akili yake, kwa hivyo akili yake ikabakia kufuata tu matamanio yake, basi hakupendelea kilichobora zaidi; huyu anakuwa ana akili pungufu.