As-Saaffaat
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
بَلْ جَآءَ بِٱلْحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلْمُرْسَلِينَ ۳۷
{37} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, akipinga kauli yao hiyo: "Bali" Muhammad "alikuja kwa haki." Yaani, kuja kwake ni kwa haki, na yale aliyokuja nayo katika sheria na Kitabu ni ya haki. "Na amewasadikisha Mitume," Yaani, kuja kwake kuliwasadikisha Mitume. Kwani lau kuwa si kuja kwake na kutumwa kwake, basi Mitume hawangekuwa wakweli. Kwa hivyo, yeye ni Ishara na muujiza kwa kila Mtume wa kabla yake. Kwa sababu walijulisha juu yake na wakabashiria kuja kwake, na Mwenyezi Mungu akachukua kwao ahadi na agano ya kwamba akiwajia, basi bila shaka watamwamini na kumsaidia, na wakachukua ahadi hiyo pia kwa umma wao. Basi alipokuja, ukweli wa Mitume wa kabla yake ukadhihirika na ukabainika uwongo wa wale waliowapinga. Na ingekuwa kwamba hakuja ilhali walikuwa wamejulisha juu ya kuja kwake, basi hilo lingekuwa la kutia dosari katika ukweli wao. Vile vile aliwasadiki Mitume; ambapo alikuja na yale waliyokuja nayo, na akayalingania yale waliyoyalingania, na akawaamini, na akajulisha juu ya usahihi wa ujumbe wao, unabii wao na sheria yao.