پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yaseen
سورهٔ ۳۶

Yaseen

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۲

وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِۦ مَا يَرْكَبُونَ ۴۲

{42} "Na tukawaumbia" hawa waliokuja baada yao "kutoka mfano wake;" yaani, mfano wa merikebu ile, "wanavyovipanda." Akawa ametaja neema yake juu ya baba zao kwa kuwabeba kwenye merikebu. Kwa sababu neema waliyopewa wao pia ni neema kwa dhuria zao. Mahali hapa ni mojawapo ya mahali pagumu sana kwangu katika kutafsiri. Kwa maana, yale waliyotaja wafasiri wengi kwamba kinachomaanishwa hapa na dhuria ati ni baba zao si jambo la kawaida katika Qur-ani, kutumia neno “dhuriya” kwa mababa. Bali, katika maana hiyo kuna utata, na kuyaondoa maneno kutoka katika mada yake, jambo ambalo linakataliwa na maneno ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, na makusudio yake ya kuwabainishia waja na kuwawekea mambo wazi. Kisha kuna uwezekano mwingine bora zaidi kuliko huu, ambao ni kwamba kinachomaanishwa hapa na dhuria ni jenasi yote, na kwamba walimaanishwa wao wenyewe. Kwa sababu wao ndio kizazi cha kibinadamu. Lakini maana hii inapingwa na kauli yake: "Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda." Lakini ikiwa maana ya kauli yake, "Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda" ni ngamia ambao ndio merikebu za nchi kavu, basi maana hii ya jenasi inakuwa nyoofu na ya wazi kabisa. Walakini, maneno haya pia yanabaki kuwa ya kutatanisha. Kwani, ikiwa maana hii ingekuwa ndiyo iliyokusudiwa, basi angesema: 'Na Ishara kwao ni kwamba tuliwabeba katika merikebu iliyosheheni, na tukawaumbia mfano wake wanavyovipanda.' Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi uhakika wa hali hii. Nilipofikia mahali hapa katika kuandika; nikadhihirikiwa na maana ambayo haiko mbali na yale aliyokusudia Mwenyezi Mungu. Nayo ni kwamba yule anayejua utukufu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maelezo yake kamili katika kila njia kinapoeleza mambo ya sasa, yaliyopita na yajayo, na kwamba katika kila maana anataja ile ambayo ni ya juu kabisa na iliyo kamilika kabisa, na pindi zilipokuwa merikebu ni miongoni mwa ishara zake, Mwenyezi Mungu Mtukufu, na neema zake juu ya waja wake tangu alipowaneemesha kwazo, kwa kuzisoma mpaka Siku ya Kiyama, na zimeendelea kuwepo wakati wote mpaka zama za wale walioongeleshwa na Qur-ani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alipozungumza nao kwa Qur-ani, na akataja hali ya merikebu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akajua kwamba hizo zitakuwa ishara kubwa zaidi merikebu zitakuja tokea katika zama zisizokuwa zao, pale atakapowafundisha kutengeneza merikebu mbalimbali zikiwemo zile za matanga, za moto, na za angani zinazokwenda angani kama ndege na vile vile vipando vya nchi kavu, ambazo ni ishara kubwa zaidi ambayo haikuwa isipokuwa wakati wa dhuria zao, akatanabahisha katika Kitabu chake juu ya aina miongoni mwa aina za ishara zake. Akasema: "Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi iliyosheheni" wapandaji wengi na mizigo. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawabeba na akawaokoa kutokana na kuzama; kwa njia ambazo Mwenyezi Mungu aliwafundisha.