پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ar-Room
سورهٔ ۳۰

Ar-Room

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۱–۵

الٓمٓ ۱ غُلِبَتِ ٱلرُّومُ ۲ فِىٓ أَدْنَى ٱلْأَرْضِ وَهُم مِّنۢ بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ ۳ فِى بِضْعِ سِنِينَ ۗ لِلَّهِ ٱلْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِنۢ بَعْدُ ۚ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ ٱلْمُؤْمِنُونَ ۴ بِنَصْرِ ٱللَّهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَآءُ ۖ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ۵

{1 - 5} Waajemi na Warumi wakati huo walikuwa miongoni mwa nchi zenye nguvu zaidi duniani, na kulikuwa na vita na mapigano kati yao ambayo huwa kati ya nchi zinazokaribiana kwa nguvu. Waajemi walikuwa washirikina walikuwa wakiabudu moto, nao Warumi walikuwa watu wa Kitabu ambacho kilikuwa Taurati na Injili, na walikuwa karibu na Waislamu kuliko Waajemi, [kwa hivyo waumini] walikuwa wakitaka kwamba wao wawashinde Waajemi. Nao washirikina kwa sababu ya kushirikiana kwao na Waajemi katika ushirikina walikuwa wakipenda kwamba Waajemi wawashinde Warumi. Kwa hivyo Waajemi wakawashinda juu ya Warumi kwa ushindi ambao haukuumaliza ufalme wao, lakini ulifikia tu sehemu iliyokuwa karibu zaidi nao. kwa washirikina wa Makka wakafurahia hilo na Waislamu wakahuzunika. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaambia, na kuwaahidi kwamba Warumi watashinda Waajemi, "Katika miaka michache" tisa au minane na mfano wake, kwa muda usiozidi miaka kumi wala haipungui chini ya miaka mitatu. "Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake." Kwa hivyo, ushindi na nusura hautokani tu kwa kuwepo kwa sababu zake. Bali ni lazima ufungamane na mapitisho ya Mwenyezi Mungu na kadari yake. "Na siku hiyo;" yaani, siku ambayo Warumi watawashinda Waajemi, "Waumini watafurahi." "Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye." Yaani, watafurahia ushindi wao dhidi ya Waajemi, hata kama kila wote wawili ni makafiri, lakini baadhi ya uovu ni rahisi kuliko mwingine. Nao washirikina watahuzunika siku hiyo. "Naye ndiye Mwenye nguvu" ambaye ana nguvu ambayo kwayo aliwashinda viumbe wote; humpa ufalme amtakaye, na humwondolea ufalme amtakaye, na humtukuza amtakaye, na humuangusha umtakaye. "Mwingi wa kurehemu" waja wake waumini, ambapo amewawekea sababu zinazowafanya wafurahi na kuwasaidia zaidi ya namna ambayo hawakuwa wanatarajia.