پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ankaboot
سورهٔ ۲۹

Al-Ankaboot

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۵۱

أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّآ أَنزَلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَىٰ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ۵۱

{51} Na kwa kuwa makusudio yalikuwa ni kubainisha haki, Yeye Mtukufu alitaja njia yake, akasema, "Je, kwani hayakuwatosha" Kwa ujuzi wao wa unyofu wako na ukweli wa kile ulichokuja nacho, "ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki wanachosomewa?" Hii ni kauli fupi na ya kina yenye ishara mbalimbali na ushahidi wa wazi wa ajabu. Kwani ilivyotangulia kwamba Mtume alikuja nacho ilhali yeye hajui kusoma na kuandika ni katika ishara kubwa zaidi juu ya ukweli wake, na kisha kushindwa kwao kukipinga na kuwapa changamoto (wakashindwa) ni ishara nyingine. Kisha ishara nyingine ni kudhihirika kwake na wao kusomewa kitabu hiki hadharani, na kusemwa kwamba kinatoka kwa Mwenyezi Mungu, huku Mtume amekiweka hadharani katika wakati ambapo alikuwa na wafuasi wachache mno na wakawa maadui wake ni wengi, lakini hawakukificha, na wala hilo halikukata azimio lake, bali ilikitangaza mbele ya mashahidi, na ikakita kati ya aliyepo karibu na wa mbali kwamba; haya ni maneno ya Mola wangu Mlezi. Basi kuna yeyote anayeweza kuyapinga, au kumsema mfano wake, au kilicho zaidi yake? Kisha kujulisha kwake juu ya visa vya watu wa mwanzo, na Mitume waliopita, na mambo ya ghaibu yaliyotangulia na yatakayokuja baadaye, kisha yote hayo yakawa yamekubaliana na hali halisi. Kisha kulinda kwake vitabu vilivyotangulia, na kuunga kwake mkono yaliyomo ya usahihi, na kukanusha kwake mambo ya yaliyobadilishwa na ya upotofu yaliyoingizwa ndani yake. Kisha kuongoa kwake njia iliyo sawa katika amri zake na makatazo yake. Na hakikuwahi kuamrisha kitu ambacho akili ilisema, 'Laiti hakingeamrisha hiki', au kukataza kitu ambacho akili ilisema, 'Laiti hakingakataza hiki.' Bali kinakubaliana na uadilifu na mizani na hekima inayoingia akilini sawasawa kwa wenye maono na akili nzuri. Kisha kuingiliana kwake vizuri na hali tofauti tofauti na zama mbalimbali katika mwongozo wake na maelekezo yake na hukumu zake kwa namna ambayo mambo hayawezi kutengenea bila ya hicho. Yote hayo yanamtosha yule anayetaka kusadiki haki na kuitafuta. Na hakika Mwenyezi Mungu na asimtosheleze yule ambaye hakutoshelezwa na Qur-ani, na wala kipambanuzi hakikumponya. Na mwenye kuongoka kwacho na akatosheka, basi hicho kwake ni rehema na heri. Na ndiyo maana akasema, "Hakika katika hayo, zipo rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini." Kwa sababu ya elimu nyingi wanayopata kutoka humo na heri tele, na utakaso wa nyoyo na roho, na usafishaji wa itikadi, na kukamilishwa tabia, na kufunguliwa kwa kiungu siri zake.