An-Naml
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذَا وَقَعَ ٱلْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَآبَّةً مِّنَ ٱلْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ ٱلنَّاسَ كَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا لَا يُوقِنُونَ ۸۲
{82} Yaani, itakapowaangukia watu "kauli" ambayo Mwenyezi Mungu alipitisha na akaiwekea muda maalumu "tutawatolea mnyama katika ardhi" ambaye si kutoka mbinguni, na mnyama huyu "atawasemesha, ya kuwa watu walikuwa hawana yakini na Ishara zetu." Kwa kuwa watu walidhoofika katika elimu yao na katika yakini yao juu ya ishara za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu kumdhihirisha mnyama huyu ni katika ishara za kimiujiza za Mwenyezi Mungu; ili awabainishie watu yale walikuwa wakiyashuku. Na mnyama huyu maarufu ambaye atatoka katika zama za mwisho, na atakuwa katika alama za Saa ya Kiyama; kama zilivyokuja hadithi nyingi zikisimulia hivyo [Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutaja jinsi namna alivyo mnyama huyu, lakini walitaja tu athari zake na makusudio yake, na kwamba ni katika ishara za Mwenyezi Mungu; ambaye atawaongelesha watu maneno yasiyo ya kawaida wakati neno litawaangukia watu. Na wakati watakapokuwa wanazitilia shaka Ishara za Mwenyezi Mungu; na hapo atakuwa ni hoja na ushahidi kwa Waumini, na hoja juu ya wale wanaompinga Mwenyezi Mungu.]